
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William
Kisinza alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa
Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini
Marekani ambao walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna
Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
Katika kufanikisha majaribio hayo,
Dkt. Kisinza amesema kituo hicho kinaendelea vizuri na majaribio ambapo
wanatarajia mchanganuo wa utafiti huo utafanyika mwishoni mwa mwaka 2016 na
taarifa kamili itatolewa rasmi mwaka 2017 ili iweze kutumika nchi nzima na
duniani kote.
Dkt. Kisinza amesema kuwa mafanikio
ya taasisi yake yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo na taasisi nyingine za
kitaaluma ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Chuo
Kikuu cha Afya cha Kilimanjaro (KCMC), Kituo cha Kudhibiti Kuzuia na Magonjwa
cha Marekani (CDC), Taasisi ya Tiba, Dawa na usafi wa mazingira ya London
nchini Uingereza (LSHTM) na Chuo Kikuu cha Brandeis cha nchini Marekani.
Mbali na kuangalia uwezo wa vitambaa
hivyo, mradi huo unaangalia pia uwezo wa vitambaa hivyo katika kukabiliana na
upugufu wa damu kwa watoto chini ya miaka 11, uwezo wa vitambaa kupambana na
mbu sugu kwenye viatilifu vingine na pia kufanya tathmini ya gharama anazoingia
mwananchi katika kugharamikia tiba za malaria.
Kitambaa hicho ambacho huwekwa
kwenye kuta za nyumba kwandani hutumika sambamba na chandarua ili kuweza kutoa
kinga madhubuti mara mbili kumkinga binadamu dhidi ya mbu waenezao magonjwa.
Mradi huo wa majaribio wa kutokomeza
ugonjwa wa malaria umeanza kufanyiwa utafiti nchini miaka mtatu iliyopita
kuanzia 2013 na unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) chini ya
Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Malaria (PMI) ambao hadi
kukamilika kwake utarajiwa kugharibu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 3.
Kwa upande wake Meneja wa
Mawasiliano Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani ambaye pia ni Mkuu
wa msafara wa waandishi hao Dena Gudaitis amesema kuwa wamefurahishwa kuona
Tanzania ilivyosimama imara kujali afya za wananchi wake hasa watu wa kipato
cha chini ambao wengi wao wanaishi vijijini.
Katika kutekeleza wajibu wao wa
kiuandishi, waandishi hao kutoka ICFJ wanaongozwa na kaulimbiu ya taasisi hiyo
inayosema “Andaa mazingira bora ya mwandishi wa habari wa kimataifa ajaye”.
Waandishi hao wa habari wamefanya
ziara ya siku tano nchini kuanzia Mei 8 hadi 13, 2016 katika mikoa ya Dar es
salaam, Arusha na Tanga ambapo wametembelea baadhi ya zahanati katika mikoa hiyo,
familia zenye watoto walio chini ya mpango wa majaribio wa kudhibiti malaria,
vituo vya utafiti vya Korogwe na Amani pamoja na kiwanda cha kutengenezea
vyandarua cha A to Z cha jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment