Watu wengi sana wamekuwa wakivaa nguo aina ya Jeans lakiwa ni wachache sana au ambao wamewahi kujiuliza ni ipi kazi ya kile kimfuko kidogo ndani ya mfuko wa mbele wa suruali za jeans.
Tumekuwa
tukivaa nguo bila kujiuliza kwanini kimewekwa pale, je kiliwekwa pale kwa
bahati mbaya? au kimewekwa tu kama urembo na hakina kazi yoyote? Jibu ni hapana
kuna sababu ya msingi ya kimfuko kile kuwepo mahali pale.
Mfuko
ule mdogo ndani ya mfuko kubwa wa mbele kwenye suruali ya jeans uliwekwa
makusudi kwa ajili ya kuhifadhia ‘saa’ kwa wale waendesha farasi (Cowboys).
Dhumuni la waendesha farasi kuwekewa mfuko ule ni ili kuibana saa isitoke
wakati wanakimbiza farasi kwani mtikisiko huwa ni mkubwa sana.
Sasa
hivi watu wamebadilisha matumizi ya mfuko ule kwa vile wengi wa wavaaji wa nguo
hizo hawaendeshi tena farasi. Watu hutumia kuwekea fedha (sarafu), betri ndogo,
iPod, simu na vitu vingine vidogo vidogo.
No comments:
Post a Comment