SUAREZ ADAI HAKUTEGEMEA KAMA ATAWEZA KUCHUKUA NAFASI YA
MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Luis Suarez amesema hakutegemea
kuchukua nafasi ya Lionel Messi ya mshambuliaji kiongozi kama alivyofanya msimu
huu.
Suarez amekuwa akiimarika toa ajiunge na Barcelona
akitokea Liverpool na amefanikiwa kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la La Liga
mara mbili huku mwenyewe akimaliza kama mfungaji kinara.
Suarez amefunga mabao 40 katika mechi 35 za ligi
alizocheza msimu huu na kumzidi mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo katika tuzo ya Pichichi kwa kufunga hat-trick katika mchezo wao mwisho
wa msimu.
Kwasasa Messi ambaye ni mshindi wa tuzo tano za
Ballon d’Or amerudi nyuma na kushambulia akitokea upande wa kushoto ili
kumpisha Suarez nafasi ya katikati. Akihojiwa Suarez amesema hakutegemea
kucheza nafasi hiyo kwani ndio ilikuwa ikitumiwa na Messi lakini wamekuwa
wakielewana vyema ndani na nje ya uwanja.
CHELSEA WATAKA KUMSAJILI LUKAKU.
KLABU ya Chelsea inadaiwa kutaka kumsajili tena mshambuliaji wao wa
zamani Romelu Lukaku kutoka klabu ya Everton.
Chelsea walimuuza Lukaku kwa kitita cha paundi
milioni 28 kwenda Everton mwaka 2014, baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mkopo
na toka wakati huo nyota huyo amefunga mabao 61 katika mechi 127 alizocheza.
Chelsea sasa wanadaiwa kutaka kumrejesha tena
mshambuliaji huyo ingawa inadaiwa Everton watataka kulipwa ada ya paundi
milioni 61 kiasi ambacho kinadaiwa kitaweza kulipwa. Chelsea pia inawawinda
nyota wa Napoli Gonzalo Higuain na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata ili
kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
BENTEKE KUTETA NA KLOPP KUHUSU MUSTAKABALI WAKE.
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Christian Benteke anataka kufanya mazungumzo
na klabu hiyo kujadili mustakabali wake baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza
ambao haukua mzuri kama ulivyotegemewa.
Benteke amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda
klabu kadhaa katika kipindi cha kiangazi ikiwemo West Ham United baada ya
kushindwa kung’aa akiwa Anfield akifunga mabao 10 katika mechi 42 za mashindano
yote aliyocheza toka anunuliwe kwa kitita cha paudi milioni 32.5 kutoka Aston
Villa.
Kukiwa hakuna uwezekano wa kushiriki michuano ya
Ulaya msimu ujao baada ya kufungw amabao 3-1 na Sevilla katika fainali ya
Europa League juzi, Benteke amesema yeye sambamba na wachezaji wengine wana
matumaini ya kuzungumza na Jurgen Klopp kuhusu mipango ya msimu ujao. Akihojiwa
Benteke amesema anafahamu kuwa bado anatakiwa kuzoea mazingira na kwasababu
msimu umemalizika anadhani sasa ni wakati wa kukaa chini ya Klopp na kujaribu
kutafuta suluhisho kwa ajili ya msimu ujao.
KAKA NDIO MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI MAREKANI.
KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Kaka ndio mchezaji anayelipwa zaidi
katika Ligi Kuu ya Marekani-MLS, akimzidi nyota wa kimataifa wa Italia
Sebastian Giovinco na nahodha wa Marekani Michael Bradley kufuatia viwango
vilivyotolewa jana.
Kaka mshindi wa ballon d’Or ambaye anacheza katika
klabu ya Orlando City ya Florida anakunja mshahara wa dola 7,167,500 akifuatiwa
na Giovinco anayechukua dola milioni 7,115,556 huku Bradley yeye akichukua dola
milioni 6.5. Wachezaji wenye majina makubwa waliojiunga na MLS katika miaka ya
karibuni ndio wanafuatia akiwemo Steven Gerrard anayecheza Los Angeles Galaxy
anashika nafasi ya nne kwa kupokea kiasi cha dola 6,132,500.
Wengine ni nyota wa New York City FC Frank Lampard
anayekunja dola milioni sita, Andrea Pirlo dola milioni 5.9 na David Villa dola
milioni 5.6. Posted by beki3 at 5:37 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share
to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
OZIL NDIO MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA ARSENAL.
KIUNGO wa mahiri wa kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil amechaguliwa na
mashabiki kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Arsenal kutokana na kiwango cha juu
alichoonyesha msimu huu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ameshinda tuzo
hiyo akiwazidi Alexis Sanchez aliyeshika nafasi ya pili na Hector Bellerin
aliyeshika nafasi ya tatu. Ozil amekuwa katika kiwango kizuri akifunga mabao
nane na kutengeneza nafasi zingine 181 msimu huu ambazo zimechagiza kwa kiasi
kikubwa Arsenal kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Leicester
City.
Kiwango hicho pia kilimfanya Ozil kuteuliwa katika
orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA ambayo ilinyakuliwa na Riyad
Mahrez wa Leicester.
GOTZE ASHAURIWA KUONDOKA BAYERN.
KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amemshauri Mario
Gotze kuondoka Bayern Munich ili kupiga hatua zaidi katika soka lake.
Gotze mwenye umri wa miaka 23 anakaribia kumaliza
mkataba wake na Bayern na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Allianz
Arena kiangazi hiki.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshindw
akupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Bayern katika kipindi cha miaka
mitatu toka ajiunge nao akitokea Borussia Dortmund. Akihojiwa Loew amesema
Gotze ni mchezaji mzuri na hana shaka na uwezo wake lakini anadhani uhamisho
unaweza kumletea changamoto mpya na kumfanya kuimarika zaidi ya alivyo sasa.
No comments:
Post a Comment