Rais
wa klabu ya Simba Evans Aveva leo May 18 amejitokeza mbele ya waandishi
wa habari na kutoa sababu kadhaa ambazo kwa namna moja au nyingine zimeifanya
klabu yao kukosa ubingwa VPL kwa mara nyingine tena ikiwa ni msimu wao wan ne
mfululizo bila kutwaa taji hilo.
Katika hotuba yake kwa
wanahabari, Aveva amekiri kwamba malengo yao waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa FA
Cup na VP yamekwama kwa kushindwa kuchua kombe hata moja kati ya hayo. Badala
yake akatumia muda mwingi kueleza sababu ambazo zimefanya Simba kushindwa
kufanya vizuri kwenye ligi.
Wachezaji wameiangusha Simba
“Kuna wanajeshi ambao
hawakuwa tayari kulitumikia jeshi la Simba kwa mfano, kuna mchezaji ambaye kwa
makusudi au kwasababu za kimchezo alifanya makosa akafungiwa kutokana na kanuni
za mchezo na sisi kama uongozi baada ya kulitathmini hilo tukaona ni lazima
tuchukue hatua kali iki kukomesha vitendo kima vile”.
“Lakini mchezaji huyu
hata kabla ya msimu kuisha tayari ameshaondoka na kusaini kwenye klabu
nyingine. Hii inaonesha kwa kiasi gani tulikuwa na wanajeshi ambao hawakuwa na
uzalendo kwenye jeshi letu”.
“Wakati tukiwa bado
kwenye mapambano, kunamchezaji akafanya rafu ambayo ilikuwa ya kimchezo kabisa
lakini inatubidi sasa tuumize vichwa kwamba ilikuwa ni ya kimchezo au makusudi.
Baada ya faulo ile, anatoa taarifa usiku wa saa tatu kwamba kesho yake saa nne
asubuhi ataondoka kwenda nje ya nchi. Tunajaribu kufanya tathmini kwamba huyu askari
alikuwa ni mwenzetu au msaliti”.
“Wakati bado
tukiendelea kuwaza juu ya hayo, kukatokea wachezaji wengine ambao walijaribu
kuwashawishi wengine kugomea michezo yote iliyobaki wakianza na mchezo wetu
dhidi ya Majimaji”.
Ushindani mkubwa katika ligi
“Zamani maisha yalikuwa
rahisi sana, unaingia kwenye ligi unamfikiria Yanga pekeyake, wengine
unawafikiria kwasababu na wao ni timu. Sasahivi ligi imebadilika, ushindani ni
mkubwa, zamani ilikuwa ni jambo la kawaida kabisa kwenye timu kupokwa
pointi kwa kushindwa kufika kwenye kituo cha mchezo kwasababu ya ukata”.
“Sasahivi timu zile za
kawaidakawaida hazipo tena, watu wamewekeza. Kuna Geita, Mwadui, Majimaji na
Mbeya City wote hao wanawadhamini”.
Utendaji mbovu wa TFF
“Utendaji wao umekuwa
sio makini kwa mfano, upangaji mbovu wa ratiba. Kalenda huwa inajulikana mwaka
mzima lakini mwaka huu imekuwa tofauti sana, lakini ratiba mbovu imechangia
kutuathiri si Simba pekeake lakini pamoja na timu nyingine”.
Waamuzi
“Waamuzi wamechangia
kwa kiasi kikubwa kuharibu matokeo ya michezo mingi kwenye ligi, si kwa
Simba tu bali hata kwa timu nyingine. Sawa tunakubali wanachukua hatua za
kinidhamu lakini lakini zile hatua huwa hazisaidii sana timu kwasababu wakati
unamfungia mwamuzi timu inakuwa imeshapoteza ushindi”.
“Tunapoanza ligi marefa
huwa wanawekwa hadharani mapema sana kwamba timu flani itaenda kucheza na timu
flani na mwamuzi atakaechezesha mchezo huo. Lakini katika mchezo wetu wa
mzunguko wa pili dhidi ya Yanga ambayo alichezesha dadayetu kutoka Bukoba,
vilabu havikujua hadi siku mbili au tatu kabla ya mchezo”.
No comments:
Post a Comment