Kocha
mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Boniface Mkwasa ametaja kikosi chenye majina
ya wachezaji 26 kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Kenya pamoja
na ile ya kufuzu kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri.
Katika
kikosi hicho nahodha wa zamani, Nadir Haroub amerudishwa kundini licha ya awali
kutangaza kujiuzulu kuchezea timu ya taifa. Haroub ameitwa kuziba pengo la
Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano na hivyo kuikosa
mechi ya Misri Juni 4.Ikuumbukwe mapema mwaka huu Canavaro alitangaza kustaafu soka la kimataifa kwa kutoichezea Taifa Stars baada ya kuvuliwa kitambaa cha unahodha na kukabidhiwa Mbwana Samatta. Baadae beki mwingine wa Stars Aggrey Morris alitangaza pia kustaafu kuichezea Stars
Kikosi
cha Taifa Stars kitaingia kambini tarehe 23 kujiandaa na mchezo wa kirafiki
dhidi ya Kenya utakaochezwa tarehe 29 Mei jijini Nairobi.Baada ya hapo Taifa
Stars itarejea Dar kukamilisha maandalizi ya kuivaa Misri katika mchezo ambao
inahitaji ushindi wa angalau mabao matatu kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwakani.
KIKOSI
KAMILI: KIKOSI CHA STARS:
Walinda
Milango:
Deo Munish ( Yanga), Aishi Manula (Azam) Benno Kakolanya ( Prisons).
Walinzi: Juma
Abdul, Haji Mwinyi,Nadir Haroub (Yanga ), Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey
Morris ( Azam), Mohamed Tshabalala (Simba), Andrew Vicent ( Mtibwa Sugar).
Viungo: Himid
Mao, Farid Mussa ( Azam), Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohamed
Ibrahim, Shiza Kichuya ( Mtibwa Sugar ),Hassan Kabunda ( Mwadui ), Juma Mahadhi
(Coastal Union). Ismail Issa Juma ( JKU)
Washambuliaji: Elias
Maguri ( Stand United), John Bocco ( Azam) Ibrahim Hajib ( Simba), Mbwana
Samatta ( Genk GRC, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu ( TP Mazembe)
No comments:
Post a Comment