HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 19 May 2016

WAKAZI WA JIJI LA TANGA WAITAKA HALMASHAURI YA JIJI KUPIGA MARUFUKU NGOMA CHAFU ZA KOKO NA URUGUAY..



BAADHI ya wakazi wa halmashauri ya jiji la Tanga wanaiomba malmaka
inayohusika kutoa vibali kupiga marufuku upigaji na uchezwaji hadharani wa
ngoma za asili hasa zisizokuwa na staha kwakuwa zinakiuka maadili yao.

Wamesema utekelezwaji wa ombi lao hilo utasaidia kupunguza kasi ya ongezeko
la maonyesho yasiyo rasmi ya ngoma hizo mbaya hasa katika maeneo ya makazi
ambako kuna idadi kubwa ya watoto na hivyo kujifunza tabia mbaya ikiwemo
vitendo vya ngono.

Wametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti walipozungumza katika mahojiano na
Mwandishi wakidai katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la kasi
la mitindo ya za ngoma za asili mitaani ambazo zimekuwa zikivuta idadi
kubwa ya vijana wakiwemo wanafunzi na watoto kutokana na mtindo mbaya wa
chezaji wake.

Aisha Abdi mkazi wa mtaa wa Dunia Hoteli uliopo kata ya Makorora alitaja
baadhi ya ngoma zikiwemo Kigodoro, Kigoma cha Uruguay, Kijamvi na Samaki-
Kambare akidai kwamba zimekithiri kwa kuchezwa vibaya tena hadharani.

“Ngoma hizi zinaanza kuchezwa mchana kweupe hadi alfajiri ambapo katika
baadhi ya mitaa wanatumia mikusanyiko ya sherehe za harusi au  vikundi vya
vijana kupongezana ambazo wenyewe wanaita Camp… katika mikusanyiko hii
mtindo wa uchezaji wa ngoma haufai kuonwa na wanajamii hasa watoto
kwasababu vitendo vinavyofwanywa hapo ni matusi yasiyoelezeka kiasi cha
kusababisha baadhi yao kuvua nguo zao zote walizovaa”,
alisema.

“Jambo la ajabu ni kwamba wanacheza hadharani na wanafunga barabara zetu
bila sababu ili mradi tu wao wapate eneo la kujimwaga... hatua hii naona
kwa upande mwingine inaathiri watumiaji wa njia hizi katika maeneo hayo
kwasababu hakuna tahadhari yoyote inayotolewa na hatuna uhakika kama kweli
wanapata vibali kutoka serikalini ili kufanya maonyesho hayo”,
alisema.


Naye Ephraim Gabriel mkazi wa Chumbageni alitaja aina nyingine ya ngoma
ambayo inaambatana na wachezaji kumwagiana maji ili wacheze kama Samaki
Kambare.Alidai kwamba mtindo huo wa kucheza kama samaki aina ya Kambare nao ni
mbaya mmno kutazamwa na husababisha kelele mitaani hasa kwa wakazi wa eneo
husika kwasababu mwimbaji hutumia kipazasauti kikubwa.

“Nashauri mamlaka zinazotoa vibali vya sherehe hizo  zinazoambatana na
upigaji wa ngoma hizi zisizo na staha kwa jamii wajaribu kutathmini kwa
upya umuhimu wake kwasababu athari ni kubwa twetu... kama mzazi hata
unapoamua kuwafungia wanao wadogo ndani ili wasione uchafu unaofanywa na
wanaocheza lakini kelele ya kipaza sauti kamwe huwezi kuizuia na mbaya
zaidi zinakesha”,
alisema.


Naye Kijana Zubeda Msema mkazi wa Ngamiani Kusini alisema pamoja na mambo
mengine kuna haja kwa mamlaka husika ikiwemo serikali kupiga marufuku ngoma
za aina hiyo ikibidi kuwakamata na kuwachukulia hatua wahusika ili
kuwawezesha wananchi kuendelea kutunza maadili.

“Pamoja na kwamba idadi kubwa ya watu wanaovutwa na ngoma hizo ni vijana
wenzangu lakini ki ukweli ni mbaya kwasababu huwezi kutazama ukiwa na mtu
mzima unayemheshimu  jambo linguine upigaji wa ngoma hizi bila mpangilio
unaathiri sana wanafunzi wa maeneo husika kwasababu wanalazimika kutumia
muda wao mwingi kutazama na kucheza badala ya kuzingatia masomo nashauri
hatua zichukuliwe haraka ili kutunusuru”,
alisema.

No comments:

Post a Comment