
Akizungumza kwa tabu na mwandishi wa
habari hizi kutokana na maumivu aliyoyapata akiwa katika Wodi ya
akinamama Hospitalini hapo , Fatma Omar Hassan alimtaja kijana aliyehusika na
kitendo hicho kuwa ni Ali Abdalla .
Aidha alikana kuwa na uhusiano
wa mapenzi na kijana huyo , licha ya kwamba amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu
akimtaka kimapenzi lakini hakukubaliana na matakwa ya kijana huyo .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini
Pemba Hassan Nassir Ali amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba
limetokea april 9 na Jeshi la Polisi linamshikilia kijana Ali Abdalla Ali
anayetuhumiwa kuhusika na shambulio hilo .
Kamanda Nassir alisema kuwa
mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili .
Hivyo aliwataka wananchi kuacha
kujichukulia sheria mikononi mwao , bali waafuate taratibu kwa kuwasiliana na
Jeshi la Polisi kwa hatua za kisheria kwani lipo kwa ajili ya kulinda usalama
wa wananchi pamoja na mali zao.
No comments:
Post a Comment