HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA
....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

.....tumia fursa yako vizuri....
Pages
Wednesday, 2 March 2016
MBUNGE "MAJI MAREFU" AWATAKA WANANCHI KUVUNJA MAKUNDI YA KISIASA NA KUFANYA KAZI.
MBUNGE wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stivn Ngonyani (CCM) amewataka wananchi wa jimbo hilo kushirikiana na kuacha makundi na kuijenga Korogwe katika nyanja mbalimbali za kilimo na Uchumi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana uwanja wa sokoni mji mdogo wa Mombo, Majimarefu aliwataka wananchi kuvunja makundi ya ushabiki wa ksiasa na badala yake kuijenga Korogwe kimaendeleo.
Alisema wananchi wa Korogwe ambao wengi ni wakulima wa kilimo cha mbogamboga na matunda pamoja na kilimo cha mkonge, wako na nafasi nzuri ya kuboresha maisha yao kwa kujiongozea kipato kupitia kilimo cha mbogamboga na zao la mkonge.
“Ndugu zangu wananchi wa mji mdogo wa mombo nimekuja hapa kuwashukuruni kwa kunichagua kwa mara ya pili kuwa mbunge wenu, niseme kuwa uchaguzi umeisha na sasa niwajibu wetu wa kushirikiana kufanya kazi” alisema Majimarefu na kuongeza
“Wakati wa kampeni mengi yamesemwa juu yangu na mwisho wa siku sanduku la kura lilijibu, ila niseme hata ambao hawakunichagua wote ni wananchi wangu na niko tayari kufanya kazi nao lengo ni kuleta maendeleo” alisema
Mbunge huyo ambaye mara nyingi hujiita Mganga wa kienyeji, aliombwa na Diwani wa kata ya Mombo, Halima Juma (CCM) kumtaka kipindi hiki akiwa mbunge kuhakikisha mji huo unapata hadhi ya kuwa halmashauri ya mji.
Diwani huyo alimtaka pia Majimarefu baada ya kufanikisha upelekaji umeme vijijini na uchimbaji wa kisima kuzichonga barabara zitokazo kwa wakulima ili kuwapa unafuu nyakati za mvua.
Alisema vipindi vya mvua wakulima wa mazao wamekuwa na wakati mgumu na kuingia gharama kubwa hivyo kuuza kwa hasara hivyo kuchongwa kwa barabara hizo itakuwa msaada kwa wakulima na wafanyabiashara.
“Mheshimiwa mbunge tunatambua michango yako kwa hali na mali na umekuwa ukiwatetea wananchi wako, kwa hayo na mengine lakini pia tunakuomba utupiganie mji wetu wa Mombo kuwa halmashauri ya mji” alisema Halima
Alimtaka mbunge huyo kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi na ya wafadhili pamoja na kuziba mianya ya ubadhrifu ili kuhakikisha pesa itolewayo inatumika kama ilivyopangwa.
CHANZO:TANGA KUMEKUCHA BLOG..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment