POLISI mkoani Tanga
inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa askari wa upelelezi.Wanaoshikiliwa
ni mkazi wa mjini Korogwe, Richard Ruther ‘Mhina’ (40) ambaye ni mmiliki wa
bastola namba GBT 552 inayodaiwa kufanya unyang’anyi na kisha kusababisha
mauaji ya askari na raia mmoja.
Mwingine
ni Hamidu Rajabu ‘Wad’ (44) mkazi wa Kabuku wilayani Handeni ambao kwa pamoja
wanadaiwa kutoa rushwa ya Sh milioni tao kuzuia askari kuendelea na upelelezi
kuhusu tukio la ujambazi lililotokea Februari 14 mwaka huu Barabara ya sita
jijini Tanga na kusababisha kukamatwa kwa bastola hiyo inayomilikiwa na Mhina.
Kamanda
wa Polisi mkoa, Mihayo Msikhela alisema jana kwamba, watu hao walikamatwa
jijini Tanga Februari 26 mwaka huu saa 10.50 jioni wakiwa ndani ya ofisi ya
Mkuu wa Upelelezi baada ya kuwekewa mtego na askari. (PICHA NI MAFANO)
No comments:
Post a Comment