Mtu
tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria, amepanda katika orodha ya
mabilionea duniani inayotolewa na jarida la Forbes, -utajiri wake ukifikia dola
bilioni 15.4. Bwana Dangote amepanda hadi nafasi ya 51, ikilinganishwa na
nafasi ya 67 mwaka 2015, alipokuwa na utajiri wa dola bilioni 14.7.
Dangote ni
muasisi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement, ambayo ni mzalishaji mkubwa
wa saruji barani Afrika. Mtu wa pili kwa utajiri barani Afrika ni Mike Adenua,
pia kutoka Nigeria ambaye ana utajiri wa dola
bilioni 10, huku mfanyabiashara wa almasi Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini
akishika nafasi ya tatu, akiwa na dola bilioni 6.6, kwa mujibu wa Forbes.
Matajiri
hao- katika orodha ya mabilionea duniani,- bwana Adenua yupo katika nafasi ya
103, na bwana Oppenheimer katika nafasi ya 174. Bilionea kijana kutoka Tanzania
Mohammed Dewji yupo katika nafasi ya 1577, akiwa na utajiri wa dola bilioni
1.1.
Kwa
orodha kamili ya watu wenye 'kisu kikali' duniani, bofya hapa:
http://www.forbes.com/billionaires/list/…
No comments:
Post a Comment