CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema licha ya
kutangaza kususia uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, pia
hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kijitoupele, mkoa wa Mjini
Magharibi, Unguja utakaofanyika sambamba na uchaguzi wa marudio.
Uchaguzi wa Kijitoupele umeitishwa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kutofanyika Oktoba 25 mwaka jana kutokana na
kasoro mbalimbali.
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CUF,
Hamad Masoud, aliliambia gazeti hili jana kuwa uamuzi wa kutoshiriki uchaguzi
wa marudio unafahamika na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na huo ndiyo
msimamo wa chama.
Hata hivyo, pamoja na msimamo huo wa CUF, ZEC
ilitangaza kumtambua mgombea Urais wa chama hicho, Seif Sharif Hamad.
Masoud alisema chama hicho hakitoshiriki uchaguzi
mdogo wa marudio wa Kijitoupele kwa sababu hakijaridhishwa na uamuzi wa ZEC wa
kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana ulioelezwa kujitokeza
kasoro nyingi.
"Msimamo wa CUF unafahamika
kwamba hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 sambamba na
uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kijitoupele ambao umeitishwa na NEC," alisema Masoud
.
Alisema chama chake hakitoshiriki katika uchaguzi
mdogo wa ubunge wa jimbo la Kijitoupele kwa sababu unafanyika sambamba na
uchaguzi wa marudio wa Machi 20 ambao CUF hakiutambui kama ni uchaguzi halali.
CUF ina jumla ya wabunge 27 katika majimbo ya
uchaguzi ya Zanzibar ambao wanashiriki katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mjini Dodoma, kwa hivyo haioni shida kulikosa jimbo moja la
Kijitoupele ambalo uchaguzi wake uliahirishwa Oktoba 25 mwaka jana.
Kwa hivyo NEC tunaijulisha kuhusu
uamuzi wetu," alisema Masoud. Uchaguzi mdogo wa ubunge wa
Jimbo la Kijitoupele unafanyika Machi 20 baada ya kuahirishwa Oktoba 25 mwaka
jana na NEC kutokana na kujitokeza kwa kasoro mbalimbali. Jimbo hilo ni
miongoni mwa majimbo matano mapya yaliyotangazwa na ZEC.
No comments:
Post a Comment