HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 2 March 2016

BEI ZA MAFUTA ZASHUKA NCHI NZIMA ISIPOKUWA TANGA. KISA SOMA HAPA....



MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini kuanzia leo Machi 2, 2016.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa  (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema bei ya Petroli imeshuka sh. 31 kwa lita sawa na asilimia 1.70, Dizeli sh. 114 kwa lita sawa na asilimia 7.10 na mafuta ya taa kwa sh. 234 kwa lita sawa na asilimia 13.75 ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Ngamlagosi amesema hapa nchini kwa sasa Petroli itauzwa Sh.1,811, Dizeli sh. 1,486 na mafuta ya taa sh. 1,465. kupungua kwa bei hizo kwa soko la ndani  kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.

Pia amesema hakutakuwa na mabadiliko yeyote ya bei ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga kwa mwezi huu na kwamba hiyo imetokana na kutopokea mafuta mapya kupitia Bandari ya mkoa huo katika kipindi cha Februari mwaka huu.

Ameongeza kuwa kwamujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta zitaendelea kupangwa na soko hivyo Ewura itaendelea kutoa taarifa za bei kikomi lengo likiwa ni kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa hiyo.
Alisema kwamba katika mabadiliko hayo, bei za mafuta kwa mkoa wa Tanga, zitabaki zile zile za mwezi uliopita, hiyo ni kwa sababu hakuna mafuta mapya yaliyopokelewa kwenye bandari ya Tanga.

Hata hivyo amevitaka vituo vyote vya mafuta nchini na kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

Ngamlagosi amewataka wanunuzi kuhakikisha  wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta kwa lita na kwamba stakabadhi ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo, au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

No comments:

Post a Comment