
Ratiba
ya shughuli zitakazofanyika mahakamani hapo katika vikao vyake vya kawaida,
zinaonyesha kuwa Rais wa mahakama hiyo, Jaji Agustino Ramadhani, tayari
amekwishaanza kuongoza vikao vya majaji wenzake kusikiliza kesi mbalimbali
zaidi ya 50.
Kesi ya Babu Seya ni miongoni mwa kesi zilizopangwa kusikilizwa Machi 11, mwaka huu.Mahakama hiyo ina majaji 11 kutoka nchi wanachama wa umoja wa Afrika (AU) ambapo hukutana mara nne kwa mwaka katika vikao vyake vya kawaida.
Walalamikaji hao wanaiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kumlazimisha malalamikiwa (Serikali ya Tanzania) kuwaachilia huru, kulipwa fidia na nafuu zingine ambazo itaona kuwa wanastahili kuzipata.Katika shauri hilo namba 006/2015, walalamikaji wanaiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi kwamba haki zao zimevunjwa na hivyo waachiwe huru na kulipwa fidia.
No comments:
Post a Comment