HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 29 February 2016

MBUNGE MAJI MAREFU ASAIDIA VILABU VYA MICHEZO KOROGWE VIFAA VYA MILIONI 5.



MBUNGE wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stivin Ngonyani, maarufu kama Profesa Majimarefu, ametoa jezi seti tano, mipira mitatu vyenye thamani zaidi ya shilingi laki 5 kwa timu ya mpira ya vijana wa Makuyuni Wilayani Korogwe lengo likiwa ni kukuza vipaji.

Vifaa hivyo kwa mujibu wa Mbunge huyo vimekuja kufuatia maombi ya vijana wa Makuyuni kumtaka kusaidia ili kuweza kuimarisha timu yao na kuingia ligi ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.
Alisema msaada huo hautoishia hapo lakini atapenda kuona timu hiyo inafanya vizuri ligi ngazi ya Tarafa na kuahidi kuisaidia kwa hali na mali hivyo kuwataka kuonyesha moyo na mapenzi na timu.

“Leo nawapeni jezi na mipira kumaliza kilio chenu kwani nakumbuka barua yenu muloniandikia nikiwa bungeni na mukaiacha kwa katibu wangu pale ofisini, niwaahidi kuwa mimi kama mbunge wenu nitakuwa nanyi bega kwa bega” alisema Majimarefu na kuongeza

“Nitahakikisha timu yenu inaingia mashindano ya Wilaya hadi mkoa na mimi kuwa mlezi wenu na musisite kunieleza kwa lolote” alisema

Kwa upande wake Kocha wa timu hiyo, Mbaraka Kiondo, alimshukuru mbunge huyo na kusema kuwa msaada wake huo aloutoa utatumika kama ilivyo na kumuahidi kuwa hawatamuangusha katika mashindano ya ligi.Alisema awali walikuwa wanatumia mipra mmoja huku wakiwa hawana jezi na badala yake kila mchezaji alikuwa anatumia fulana yake jambo ambalo lilikuwa kero wakati wa uchezaji na kutoelewana.

“Mheshimiwa Mbunge hatuna la kukulipa na hatuna la kusema kwani hatujui tuanze wapi ila nimalize kwa kusema asante sana na Mungu ndie atakakulipa na kukubariki” alisema Kiondo
Aliwataka wachezaji wake kuzingatia muda wa kufanya mazoezi baada ya kupata vifaa hivyo na kuwataka kupiga kambi ili kushikilia usukani wa ligi hiyo ngazi ya Tarafa na msimu wa ligi kuingia ngazi ya Wilaya.

No comments:

Post a Comment