
Watu hao
walikutwa na karatasi yenye ujumbe kwa aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Suleiman Kova ulioandikwa:
“Nasaha
kwa Kova, mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza
tutakufikia wewe.”
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas (pichani)alisema jana kuwa tukio hilo,
lilitokea Jumamosi iliyopita, eneo la Fire, jijini Arusha wakati mtuhumiwa
Athumani Kassim alipokamatwa eneo la Engosheraton akiwa na silaha na aliwataja
wenzake.
Kamanda
Sabas alisema walipopata taarifa kutoka kwa raia wema walio tilia shaka
mwenendo wa mtuhumiwa huyo ambaye alipokamatwa, alikutwa na milipuko, makoti
makubwa mawili na kofia ya kuficha uso.
“Baada ya
mahojiano, alituambia kuna wenzake wawili anashirikiana nao kufanya uhalifu na
tuliweka mtego.
“Saa 5 usiku, askari wetu wakiwa wameambatana na Kassim,
walipofika jirani kabisa na nyumba hiyo eneo la Fire, alitoa ishara na wenzake
wakaanza kuwashambulia polisi kwa risasi,” alisema
kamanda huyo.

Alisema
kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi, walikuta vitu mbalimbali ikiwamo sare tano
za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kofia tano za kuficha nyuso, vazi moja
la karate, pikipiki moja iliyobomolewa na imebandikwa namba bandia. Alivitaja
vitu vingine kuwa ni bendera mbili nyeusi zenye maandishi ya Kiarabu
zinazotumiwa na makundi ya kigaidi.
Vitu
vingine ni kisanduku cha chuma na hati ya kusafiria ya Abrahaman Athuman
Kangaa, iliyotolewa Aprili 2, 2013, simu tano za mkononi na kati ya hizo, moja
ilitambulika kuwa ni ya marehemu Mary Joseph aliyefariki kwa kupigwa risasi na
watu wasiojulikana Februari 20, mwaka huu, eneo la Engosheratoni pamoja na
kifurushi cha unga wa baruti na jambia moja.
Miili ya
majambazi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya
utambuzi.
No comments:
Post a Comment