HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 28 February 2016

MAKAMU WA RAIS BI.SAMIA AKERWA NA MGOGORO WA UMEYA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo jana.
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kumaliza haraka mgogoro wa uongozi ndani ya halmashauri hiyo, kuharakisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Alitoa agizo hilo katika Ikulu ndogo ya Tanga wakati akizungumza na viongozi baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Tanga baada ya kuwasili kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa mazingira unaoratibiwa na Unesco.

Alisema kwa kuwa uchaguzi mkuu umekwisha salama, ajenda inayopaswa kutekelezwa sasa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuwezesha wananchi kupata maendeleo.

Alisema serikali ina mpango mkubwa wa kuwekeza katika viwanda kwenye jiji la Tanga. Hata hivyo alisema endapo hakutakuwa na uongozi wa Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo, malengo hayo hayataweza kutekelezwa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akisoma taarifa, alisema mkoa umejipanga na kuweka mikakati ya kutekeleza mipango mbalimbali katika sekta za elimu, afya, maji, viwanda na mazingira kuwezesha wananchi kujipatia maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza (aliyeketi kulia).


No comments:

Post a Comment