HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 11 February 2016

WAFANYABIASHARA KUTOKA TANGA WAUAWA NA MAJAMBAZI NCHINI MSUMBIJI.



Wafanyabiashara wanne wa Tanzania wameuwa kwa kupigwa risasi kisha kuchomwa kwa vitu vyenye ncha kali nchini Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe (PICHANI) alisema tukio hilo lilitokea usiku wa Jumatatu iliyopita katika machimbo ya dhahabu, Kijiji cha Mtoro Mtupweshi Kamprigando.

Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Salum Mfanga (44) Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Yusuph Twalibu (34) na Mariam Ramadhani (30) wakazi wa Tanga na Hamisi Mkapira (40) wa Morogoro.

Kamanda huyo alisema kifo cha Mariam ambaye alifanikiwa kujiokoa, kilisababishwa na kukosa huduma ya haraka baada ya kuvunjika mguu.

Kamanda huyo alisema wafanyabiashara hao walivamiwa na majambazi waliokuwa na risasi pamoja na mapanga katika vibanda vya kubadilishia fedha nchini humo. “Miili ya wafanyabiashara hao ililetwa na ndugu zao ambao wanaishi Msumbiji,” alisema.

Wakizungumzia tukio hilo, Said Mfanga na Dotto Ramadhani ambao ni ndugu wa marehemu hao walisema baada ya kuwaua, majambazi hao waliwapora fedha pamoja na mabegi yao.

No comments:

Post a Comment