HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 14 February 2016

COASTAL WAIBUGIZA 1-0 AZAM TANGA LIGI KUU BARA.

AZAM FC imeshindwa kuiengua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC, baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Shukrani zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, ambalo linavunja rekodi ya Azam FC kutofungwa msimu huu, beki wa kulia Miraj Adam aliyetikisa nyavu za timu ya Azama kukanako dakika ya 67 ya mchezo.
Adam aliyefunga pia katika ushindi wa 2-0 Coastal Union ikivunja rekodi ya Yanga SC kutofungwa msimu huu – leo alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu pia, baada ya kuanzishiwa na beki mwenzake wa pembeni, Adeyum Saleh Ahmed.

Kipa Aishi Manula(PICHANI) ana kila sababu ya kubeba lawama kwa bao hilo, kwani alidaka mpira na kulala nao kwa muda mrefu huku akiugulia maumivu badala ya kuutoa nje kwanza na refa Vincent Mlabu kutoka Morogoro aliyesaidiwa na Gasper Ketto na Mohammed Mkono akawaadhibu Azam.

Matokeo hayo yanaifanya Coastal Union ifikishe pointi 16 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda hadi nafasi ya 13, kutoka ya 16 ilipokuwa inashikilia mkia, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 42 za mechi 17, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 43 za mechi 18 na Simba SC pointi 45 za mechi 19.

Kikosi cha Coastal Union kilikuwa
1.     Fikirini Bakari,
2.     Hamad Juma,
3.     Adeyum Saleh Ahmed,
4.     Mbwana Hamisi ‘Kibacha’,
5.     Miraj Adam,
6.     Sabo Youssouf,
7.     Juma Mahadhi,
8.     Abdulhalim Humud,
9.     Abasarim Chidiebere,
10. Ally Ahmed ‘Shiboli’/Ayoub Yahya dk78
11. Nassor Kapama.

Azam FC
1.     Aishi Manula,
2.     Shomary Kapombe,
3.     Erasto Nyoni,
4.     Said Mourad,
5.     Serge Wawa,
6.     Farid Malik/Gardiel Michael dk46,
7.     Michael Balou,
8.     Frank Domayo/Salum Abubakar dk46,
9.     Jean Mugiraneza,
10. John Bocco
11. Allan Wanga/Kipre Tchetche dk69.

Mechi Za Leo 2016-02-14
Ft
Mwadui Fc
0
 : 
0
T.Prisons
Ft
Coastal Union
1
 : 
0
Azam Fc
Michezo Inayokuja
Jumamaosi 2016-02-20
16:00
Yanga
Vs    
Simba Sc
16:00
Mgambo Jkt
Vs    
T.Prisons
16:00
Stand United
Vs    
Jkt Ruvu
16:00
Mbeya City
Vs    
Azam Fc
16:00
Majimaji
Vs    
Mtibwa Sugar
16:00
Toto Africans
Vs    
Kagera Sugar
Jumapili Februari 21
Ndanda FC v African Sports        
Mwadui FC v Coastal Union

No comments:

Post a Comment