Serikali
mkoani Kilimanjaro imeuagiza uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
(Kinapa), kuwachukulia hatua askari wanaodaiwa kuwanyanyasa wanawake wanaoingia
katika Misitu ya Nusu Maili kukata nyasi na kuokota kuni.
Mkuu wa mkoa huo, Amos Makala alitoa agizo hilo jana kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mshiri wilayani hapa.
Alisema katika ziara aliyofanya kwenye vijiji vinavyozunguka
msitu huo, wanawake wamekuwa wakilalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili,
ikiwamo ubakaji na kupigwa
wanapokutwa na askari hao wakikata nyasi kwa ajili kulisha ng’ombe na kuokota
kuni za kupikia.
“Kinapa najua wapo baadhi ya askari wenu ambao siyo
waaminifu, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili na vya kinyama wanawake
wanaoingia katika Msitu wa Nusu Maili. Kwa hiyo nawaagiza kuwachukulia hatua za
kisheria mara moja,” alisema Makala Mkuu huyo wa mkoa alisema vitendo hivyo ni
vya aibu na vya kusikitisha kwa taasisi kubwa ya umma.
“Mtu mzima hawezi kusimama kwenye hadhara ya watu wengi
namna hii na kusema uongo katika mambo makubwa kama kubakwa na kutembezwa kwenye
hifadhi siku nzima, kupigwa na
kukalishwa kwenye siafu,” alisema Makalla.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Veronica Mlay alisema
wamekuwa wakiingia katika hifadhi hiyo siku za Jumatano na Jumamosi ambazo
wameruhusiwa kukata nyasi na kuokota kuni, lakini baadhi ya askari wa Kinapa
wanapowakuta huwafanyia vitendo vya unyanyasaji.
Kaimu mhifadhi wa hifadhi hiyo, Charles Ngendo alisema
vitendo hivyo viliwahi kulalamikiwa miaka ya nyuma katika ofisi yake na
kuvishughulikia.
chanzo:Mpekuzi Blog
No comments:
Post a Comment