HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 19 February 2016

PATA TAARIFA MUHIMU ZA LIGI KUU TZ BARA KABLA YA MCHEZO WA KESHO "SIMBA VS YANGA"


Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea wikiendi hii mzunguko wa 20 kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali huku Jumamosi michezo mitano ikichezwa kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu katika ligi hiyo.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Yanga SC v Simba SC watakua wakichuana kusaka uongozi wa Ligi hiyo katika mchezo namba 153, huku Mgambo Shooting wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City watawakaribisha Azam FC katika uwanja wa Sokoine mjini humi, mjini Shinyanga chama la wana Stand United watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Kambarage, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Jumapili Ndanda FC watakua wenyeji wa African Sports uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mwadui FC watakua wenyeji wa Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga, huku wana lizombe Majimaji FC wakicheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.


WASEMAVYO MAKOCHA WA SIMBA  NA YANGA, KABLA YA MCHEZO WA KESHO.
Kocha wa Simba, Jackson Manyanga, amesema itafanya vizuri dhidi ya Yanga katika mechi ya keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa kutokana na kuimarika kwa kikosi chake.

Timu hizo zitachuana katika mechi hiyo ya pili ya watani wa jadi msimu huu itakayochezeshwa na refa mwanamama Jonesia Rukyaa kutoka Kagera.

Akiwa kambini Morogoro jana mchana, Mganda huyo alisema kuwa kutokana na kiwango kizuri cha wachezaji, kujitoa pamoja na morali yao, anaamini watapata ushindi dhidi ya mabingwa haoi watetezi.

Alisema timu yake haitarajii kitu kingine zaidi ya ushindi katika mechi ambayo ndiyo itatoa dira ya timu itakayotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu.

 “Wachezaji wetu wako tayari kwa mechi ya watani, Yanga ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri na wenye uzoefu na kucheza dhidi yao mara zote ni mechi ngumu, lakini tuko tayari kuwakabili wikendi hii,” alisema.

Wakati Mayanja akitoa tambo hizo, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema jana kuwa hawaoni sababu kuntu kwa kikosi chao kupoteza mechi ya Jumamosi kutokana na maandalizi mazuri wanayoendelea kuyafanya visiwani Pemba pamoja na kurejea uwanjani kwa nyota wao waliokuwa majeruhi.

Mwambusi, kocha wa zamani wa Mbeya City FC, alisema anajua mechi itakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Simba ambacho kimeshinda mechi zote saba zilizopita za VPL(sita chini ya Mayanja).

“Tunakijua kile ambacho kinawapa matumaini ya kushinda mchezo wa Jumamosi, lakini tumejipanga kuepukana nacho na kushinda kama ilivyokuwa mzunguko wa kwanza. Tutaonyesha ubora wetu siku hiyo uwanjani,” alisema Mwambusi.

Takwimu za Nipashe zinaonyesha kuwa katika mechi 12 zilizopita za watani wa jadi Ligi Kuu tangu mwaka 2010, Simba inayoongoza msimamo wa VPL kwa sasa ikiwa na mtaji wa pointi 45, imefunga mabao 15 dhidi ya Yanga, lakini Wanajangwani wameshinda mara nne huku wapinzani wao wakiibuka na ushindi mara tatu.

Ushindani mwingine mkali unaosubiriwa Jumamosi utawahusisha kinara wa Hamis Kiiza wa Simba na Amissi Tambwe wa Yanga wanaowania kiti cha Simon Msuva cha Mfungaji Bora wa msimu.

Kiiza ametupia mara 16 katika mechi 19ambazo
 Simba imecheza msimu huu wakati Tambwe yuko nyuma ya Mganda huyo kwa mabao mawili.



Orodha ya Wafungaji Bora
Rn
Player Name
Timu
Goal
1
Hamisi Kiiza
Simba SC
16
2
Amisi Tambwe
Yanga SC
14
3
Donald Ngoma
Yanga SC
10
4
Jerema Juma
T.Prisons
10
5
Elias Maguli
Stand United
9
6
Ibrahim Ajibu
Simba SC
8
7
Kipre Tcheche
Azam FC
8
8
Shomari Kapombe
Azam FC
7
9
Atupele Green
Ndanda FC
6
10
John Bocco
Azam FC
6
11
Saimon Msuva
Yanga SC
6
12
Edward Christopher
Toto Africans
5
13
Fully Zully Maganga
Mgambo JKT
5


Rn
Timu
P
W
D
L
F
A
Gd
Pts
1
Simba Sc
19
14
3
2
35
11
24
45
2
Yanga
18
13
4
1
42
9
33
43
3
Azam Fc
17
13
3
1
31
11
20
42
4
Mtibwa Sugar
18
9
6
3
21
12
9
33
5
T. Prisons
18
8
6
4
18
17
1
30
6
Mwadui Fc
19
8
5
6
19
16
3
29
7
Stand United
18
9
2
7
18
15
3
29
8
Mbeya City
19
5
6
8
20
23
-3
21
9
Toto Africans
19
5
6
8
18
27
-9
21
10
Ndanda Fc
19
4
8
7
17
19
-2
20
11
Mgambo Shooting
19
4
5
10
15
24
-9
17
12
Coastal Union
19
3
7
9
13
20
-7
16
13
Kagera Sugar
19
4
4
11
10
22
-12
16
14
African Sport
19
4
4
11
6
19
-13
16
15
Majimaji Fc
19
4
4
11
11
32
-21
16
16
Jkt Ruvu
19
3
5
11
18
30
-12
14

No comments:

Post a Comment