Tanga,
KOCHA Mkuu wa Muheza United, John Kingi, amesema kipigo walichokitoa kwa Small
Prison ya Tanga ni salamu kwa wapinzani wao watakaokutana fainali na kutoa
salamu kuwa kombe la ligi ngazi ya Mkoa
litaenda Muheza.
Akizungumza mara baada ya kipenga cha mwisho uwanja wa
Mkwakwani juzi, Kingi aliwapongeza wachezaji wake na kuwataka kuongeza mazoezi
bila kukosa i na morali wa ushindi siku ya fainali Febr 28.
Alisema mchezo huo ulipoanza
alikuwa na hofu kutoka na wapinzani wao kutumia pasi ndefu na mipira ya juu hivyo kuubadilisha kwa
kutumia mfumo wa 3, 5 , 2 na kuwachanganya wachezaji wa Small Prison.
“Mpira
ulipoanza tu nilingia hofu kwa mfumo wao wa kutumia pasi ndefu na pasi za juu,
ndipo wachezaji wangu nikawapanga kwa mfumo mwengine na kupata mabao ya chap
chap” alisema Kingi na kuongeza
“Sasa
mawazo na akili yetu iko kwenye fainali ambayo tunakutana na majirani zetu wa
Korogwe United, tunawajua kuwa ni wazuri sio wa kuwabeza ila niseme kuwa nasi
tunajipanga” alisema
Alisema kwa sasa wataweka kambi kuhakikisha wachezaji wake
wanafanya mazoezi mfululizo na kuwajenga kimwili na kimchezo hadi siku ya
fainali na kombe hilo kwenda Muheza.
Kwa upande wake, kocha
wa Small Prison ya Tanga, Msafiri Hassan, amemlaumu refarii na kusema
aliwanyima nafasi za kufunga ila kwa sasa anajipanga msimu wa ligi kwa kufanya
usajili wa nguvu.
Alisema
mwamuzi aliwanyima nafasi za kuelekea kufunga mara tatu na kusema
mazingira hayo yaliwanyong’onyeza wachezaji wake na kupoteza morali wa uchezaji
uwanjani.
“Tuseme
ligi imeisha licha kuwa tutacheza na Jeshi Worrias kusaka nafasi ya tatu,
malengo yetu ilikuwa ni kuingia fainali na matokeo ndio kama haya yaliyotokea
kwa kweli inauma sana” alisema Hassan
Alisema kipindi cha kuisha kwa ligi kazi ambayo ataifanya ni
kutafuta wachezaji wenye kipaji ili kukisuka kikosi ambacho kitakuwa moto na
kuhakikisha kombe hilo liwe la kwao.
Alisema usajili wake hautokuwa mkubwa kama watu
wanavyofikiria bali kutakuwa na mabadiliko madogo sehemu ya beki, kiungo na
ushambuliaji na kudai kuwa hatakurupuka kufanya usajili huo.
No comments:
Post a Comment