Kufuatia
agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa
makontena 349 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la
Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika
na wizi huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP)
Diwani Athumani (Pichani) amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea
katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili
ambao wamehusika na wizi huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na
mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi
na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma
mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki,
Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi. Habib Mponezia,
Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi.
Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw.
Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis
Omary.
Aidha Kamanda Athumani amewaomba
wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi
la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.
Chanzo:Mpekuzi Blog
Chanzo:Mpekuzi Blog
No comments:
Post a Comment