John
Cena.
Nyota
wa mieleka ya maonyesho ya WWE, John Cena, amedai kuachana na shoo hiyo
iliyokuwa ikioneshwa kwenye televisheni na kufanya kitu kingine tofauti.
Cena, amedai kuwa amekuwa katika ulimwengu wa mieleka kwa zaidi ya miaka 13 na kusema kuwa amechoshwa na aina hiyo ya maisha.
Sambamba na hilo amedai kuwa amepata dili la shoo nyingine ya televisheni ya Fox itakayokuwa ikionyesha maisha yake halisi itakayoenda kwa jina la ‘American grit’.
Cena amesema kujitoa kwake kutafungua milango kwa wakali wapya WWE na kudai kuwa sasa anataka kuweka nguvu zake pia katika uigizaji wa filamu.
KOBE
BRYANT KUSTAAFU KIKAPU MWAKANI.
MCHEZAJI
nyota wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA, Kobe Bryant ambaye
anahesabiwa kama mmoja ya wachezaji bora kabisa katika historia, anatarajiwa
kustaafu mchezo huo mwishoni mwa msimu.
Bryant amefunga vikapu 32,683 katika kipindi
cha miaka 20 alichoichezea timu ya Los Angeles Lakers na kumfanya kushika
nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa wakati wote wa NBA.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye
ana medali za dhahabu za mashindano ya Olimpiki, amekuwa akisumbuliwa na
majeruhi katika misimu ya karibuni na kumfanya kuwa chini ya kiwango msimu huu
akiwa na Lakers.
Bryant alitajwa kama Mchezaji Mwenye Thamani
Zaidi wa NBA mwaka 2008 na amewahi kuchaguliwa katika kikosi cha NBA All-Star
kwa nyakati 17 tofauti. Mchezo wa mwisho wa Bryant unatarajiwa kuwa dhidi ya
Utah Jazz utakaochezwa Aprili 13 mwakani.


No comments:
Post a Comment