Na Masanja Mabula -Pemba
Wakaazi wa Kisiwa cha
Fundo wanaokubaliana na sera za Serikali ya kuimarisha uchumi wake kupitia
sekta ya Utalii waanza kuonja machungu ya kususiwa pamoja na kutopewa huduma za
kijamii ikiwemo za mahitaji ya kila siku za nyumbani .
Tayari wananchi hao wamekuwa na wakati
mgumu kutokana na kukosa huduma ya chakula madukani pamoja na huduma za usafiri
wa kutoka Kisiwani humo kwenda Wete .
Wakizungumza na mwandishi wa habari
hizi baadhi ya wananchi ambao wameonja joto ya kususiwa wameiomba serikali
ichukua hatua za haraka za kukumaliza mgomo huo ili waweze kuendelesha maisha
yao bila ya hofu .
Wamesema kuwa baadhi ya wananchi tayari
wamewahi kushushwa katika vyombo vya baharini licha ya kwamba walikuwa na
mizigo na watoto wachanga .
"Mimi nilishushwa kwenye mashuwa
nikiwa na mtoto mchanga pamoja na mizigo nikiwa maji ya shingoni , nilijikokota
na kwa bahati ilikuja boti ya mwekezaji kunichukua baada ya kupewa taarifa na
wasamiria wema " alieleza mmoja wa wahanga hao .
Aidha wapo baadhi yao ambao wamepata
adha ya kutomeshwa na mbwa na na vijana jambo ambalo linaweza kusababisha
kuwepo na uvunjfu wa amani kwa wakaazi wa Kisiwa hicho .
Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ametakiwa wafanyabishara hao kuendesha
biashara zao kwa mujibu wa sharia na leseni zao kwa kuhakikisha kwamba
wanatoahuduma kwa wananchi wote bila ya ubaguzi Amesema kuwa Serikali ya Mkoa
haiwezi kukaa kimiya wakati wananchi wake wanaendelea kuteseka kwa kukosa
kupatiwa huduma na mahitaji muhimu ya kijamii .
"Serikali haiweze kuvumilia
matendo ya aina hii kuendelea kutokea , ni vyema wafanyabiashara kufuata sheria
ambazo zimo katika mikataba ya biashara yao kwa kuhakikisha wanatoa huduma
kwa wote bila ya ubaguzi " alisema .
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema iwapo
wafanyabiashara hao wataendelea kukaidi agizo hilo , hatua za kisheria
zitachukuliwa na taasisi husika ikiwa ni pamoja na kupokonywa leseni za
biashara zao .
"Iwapo wataendelea na mgomo huo
basi hatua za kuwapokonywa leseni za biashara zao zitachukuwa na vile vyombo
vya baharini vitapandishwa juu na serikali itaweka chombo kwa ajili ya wananchi
wote wa Fundo " alifahamisha .
Mgomo huo umekuja kufuatia Serikali
kuruhusu mwekezaji kuwekeza katika Kisiwa hicho huku baadhi ya wakaazi wake
wakiwa wanapinga kuwepo na mwekezaji katika Kisiwa hicho .
No comments:
Post a Comment