Mkuu wa mkoa wa
kaskazini Pemba mhe omar khamis Othman amewataka watendaji wa Idara ya Upimaji
Pemba kuwashirikisha wananchi wakati wa upimaji wa ardhi ili kuepusha migogoro
isiyokuwa ya lazima .
Amesema kuwa migogoro mingi ya ardhi
inayotokea katika mkoa huo inasababishwa na watendaji wa Idara ya Upimaji
kutowashirikisha wananchi wakati wa upimaji .
|
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba
Mhe Omar Khamis Othman
|
Kauli hiyo ameitoa huko ofisini
kwake wete wakati akizungumza na watendaji wa Idara ya Upimaji Pemba , Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni katika kikao cha kusuluhisha mgogoro wa ardhi
iliyoko Makangale kati ya Mzee Ali Said na mwakilishi wa Mhe Samiya Suluhu
Hassan .
Aidha mkuu huyo wa Mkoa amefahamisha
kwamba wananchi wanaozitumia ardhi hizo wanapaswa kushirikishwa wakati wa
upmaji kwa kulipwa fidia ya vipando na mazao yao
yaliyomo katika maeneo yanayopimwa .
Naye katibu Tawala Wilaya ya
micheweni Bw Hemed Khalid Abdalla ameitaka Idara ya Upimaji Pemba kusaidia
kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha kwamba wanafuata misingi ya
utawala bora ya ushirikishwaji .
Amesema kuwa migogoro ya ardhi ambayo
inajitokezwa katika Wilaya ya Micheweni inaweza kuzuiwa iwapo Idara ya Upimaji
itawashirikishwa wnanchi wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi zake .
No comments:
Post a Comment