![]() |
|
Vijana
wanaoishi kwenye nyumba za kurekebisha tabia (SOBA HOUSE) iliyoko Pemba
|
Na Masanja Mabula .PEMBA
Vijana wanaoishi kwenye nyumba za
kurekebisha tabia (SOBER HOUSE)baada ya kuamua kuachana na utumiaji wa
dawa za kulevya Wilaya ya wete pemba wameiomba Serikali kuwapatia dawa za
kinga ya maji ili kuwanusuru kupata maradhi ya mripuko .
Mratibu wa nyumba
hizo abdulwahid salim said amesema kuwa kutokana na mvua za masika ambazo
zinaendelea kunyesha kwa sasa uwezekano wa kupata maradhi ya mripuko ni mkubwa
iwapo hakutachukuliwa hatua za haraka .
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi huko katika nyumba namba moja iliyoko Limbani ,
amesema kuwa kwa sasa baadhi ya vijana wamekuwa wakabililiwa na matumbo ya
kuharisha yanayotokana na kunywa maji ambayo hayako salama kwa afya za
wananchi .
Amesema kuwa pamoja
na kwamba wanatumia maji ya bomba lakini yanahitaji kuchemshwa kabla ya
kutumika jambo ambalo linawawia vigumu kutokana na gharama kubwa hivyo wameomba
kupatiwa wate guard ili waweze kunusuru kupata maradhi ya mripuko .
"Katika kipindi
hichi ambapo mvua za masika zinaendelea kunyesha uwezekano wa kupata
maradhi ya mripuko ni mkubwa , hivyo tunaomba kupatiwa dawa ya maji ili kuweza
kunusuru afya zetu " alieleza .
Aidha abdulwahid
ameeleza kwamba mbali na kukabiliwa na changamoto hiyo lakini vijana wanaoishi
katika nyumba hizo wanaweza kupata maaedhi ya kuambukiza kutokana na mgodoro
wanayotumia kuwa ni muda mrefu .
Amesema kuwa magodoro
hayo yanaendelea kutumika tangu miaka mitatu iliyopita ambapo vijana wanaoingia
na kutoka wanayatumia bila ya kujua athari zinazopweza kuwapata .
"Magodoro
yaliyopo ni ya zamani na vijana wanaiongia na kutoka kila siku , pia tunahofu
kwamba kunaweza kutokea maradhi ya kuambukiza kutokana na magodoro yanayotumika
na vijana " alifahamisha .
Kutokana na
changamoto hiyo ametupa lawama kwa Viongozi wa majimbo Wabunge na Wawakilishi
kwa kushindwa kuzitembelea nyumba hizo na kuwashukuru Viongozi wakuu wa Nchi
kwa kuwa na utaratibu wa kuwatembelea mara kwa mara .
"Tunatambua
uwepo wa viongozi wa majimbo Mbunge na Mwakilishi , lakini sisi hatujawaona
kututembelea ambapo viongozi wakuu wa nchi wamekuwa na kawaida ya kututembelea
lakini viongoji wa majimbo hatuwaoni " alisema .
Wilaya ya Wete
ina nyumba mbili ambazo zinatoa programu kwa vijana wanaoacha matumizi ya dawa
za kulevya ambapo jumla ya 53 kutoka Bara na Visiwani wanaendelea na programu
zao katika nyumba hizo .

No comments:
Post a Comment