Tume
ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa, haitaweza kufanyika tena tarehe 30 April hadi hapo
itakapotangazwa tarehe nyingine tena.
![]() |
| Jaji Lubuva |
Akizungumza na waandishi .wa habari jana
mchana, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi , Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema
sababu ya kuhairisha kura hiyo April 30 ni kutokana na kutokamilika kwa zoezi
la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura kutokana na changamoto za
mashine za BVR.
Jaji Lubuva amesema zoezi la uandikishaji mkoa wa Njombe litakamilika April 18 na baada ya hapo itafuatia mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mtwara na Lindi . Vifaa vya kuandikishia (BVR kits) nyingine 248 zitawasili ndani ya wiki ijayo na vingine 1600 vitafuata baada ya muda mfupi.

Pia, amesema kama vifaa vya
kuandikishia vitafika vyote zoezi la uandikishaji litakamilka ifikapo mwezi julai mwaka huu.
Jaji Lubuva ameainisha kuwa Gharama za vifaa vyote vilivyoagizwa kwaajili ya vifaa vya kuandikishia (BVR kits) ni dola za Kimarekani milioni 72 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 13,338,520,536.
Jaji Lubuva ameainisha kuwa Gharama za vifaa vyote vilivyoagizwa kwaajili ya vifaa vya kuandikishia (BVR kits) ni dola za Kimarekani milioni 72 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 13,338,520,536.

No comments:
Post a Comment