Wiki iliopita ilitolewa takwimu za wachezaji
wakali (bora) kwenye kila idara yaani kuanzia makipa, mabeki, viungo mpaka
washambuliaji mwaka huu 2015 tokea uanze.
Sasa kwenye washambuliaji wakali kwa sasa barani Ulaya, mchezaji
bora duniani Cristiano Ronaldo, hakuwepo kwenye 10 bora na wala hakuwepo kwenye
20 bora. Jamaa amekamata namba 29.
Ajabu
kweli kweli, lakini ndio hivyo. Kwa washambuliaji wakali tokea mwaka huu uanze
huko barani Ulaya, ni mpinzani mkubwa wa Cristiano, Messiiiiiiiii…., akifuatiwa
na Arjen Robben wa Bayern Munich.
Jana kocha
wa Real Madrid akakiri kuwa ni kweli mchezaji wake ameshuka kiwango, ila
atarudi tena hivi karibuni.
Cristiano
amepiga kimya, na akawajibu watu watoaji wa takwimu.
Timu yake ya Real Madrid juzi ilishinda 9-1 kwenye La Liga huku yeye akipiga magoli matano peke yake, yakiwemo magoli matatu (hat-trick) ya ndani ya dakika 8.
Timu yake ya Real Madrid juzi ilishinda 9-1 kwenye La Liga huku yeye akipiga magoli matano peke yake, yakiwemo magoli matatu (hat-trick) ya ndani ya dakika 8.
Kama
kawaida ya Cristiano na Messi, wakifunga basi kuna rekodi au takwimu fulani
wanakuwa wamefikia au kuvunja na kuweka mpya.
Sasa hebu tucheki magoli hayo matano ya Cristiano yametuletea vitu gani .
Sasa hebu tucheki magoli hayo matano ya Cristiano yametuletea vitu gani .
1] Hii ni
mara ya kwanza kabisa kwa mchezaji huyo kufunga magoli matano tokea ajiunge na
Real Madrid na ni hat-trick yake ya upesi zaidi.
2] Ni
mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga hat-trick ndani ya dakika nane bila
penati tokea mwaka 1960. Lakini si kwamba ndie wa kwanza kufunga magoli matano
peke yake kwenye klabu hiyo.
3] Sasa
amefunga hat-trick ya 24 kwenye La Liga ndani ya misimu sita tokea ajiunge na
Real Madrid na kumfikia Lionel Messi. Wote wawili wana hat-trick sawa sasa
kwenye Ligi Kuu ya Hispania. Messi amefunga hat-trick zake ndani ya misimu
misimu 11.
Wastani wa
Cristiano hapa ni mzuri sana. Hii ina maana kuwa kila msimu ana uwezo wa
kufunga hat-trick 4, katika miaka sita yake ndani ya Real Madrid, wakati Messi
ana wastani wa hat-trick 2 kwa msimu mmoja kwa miaka yake 11 mpaka sasa ndani
ya Barcelona.
4] Ndie
mchezaji mwenye hat-trick nyingi ndani ya Real Madrid kwenye La Liga.
5] Hat-trick
yake ya leo pia imemfanya afikishe hat-trick 28 jumla tokea ajiunge na Real
Madrid.
Hii ina
maana katika michuano yote aliocheza na timu hiyo.
Na kwa idadi hizo za hat-trick 28, basi Cristiano amemfikia mkongwe wa zamani Alfredo Di Stefano wa timu hiyo. Yaani wote wana hat-trick sawa kila mmoja kwenye historia ya klabu hiyo.
Na kwa idadi hizo za hat-trick 28, basi Cristiano amemfikia mkongwe wa zamani Alfredo Di Stefano wa timu hiyo. Yaani wote wana hat-trick sawa kila mmoja kwenye historia ya klabu hiyo.
Di Stefano
ana hat-trick 22 kwenye La Liga, huku 6 nyingine zikiwa kwenye michuano ya
Ulaya.
Yeye na Di
Stefano ndio wachezaji wenye hat-trick nyingi zaidi kwenye historia ya Real
Madrid.
6] Kwa
ujumla hiyo ni hat-trick ya 31 kwa mchezaji huyo tokea aanze kucheza soka la
kulipwa akiwa na klabu tofauti alizopitia pamoja na timu ya taifa ya Ureno.
7] Mpaka
sasa amefunga jumla ya magoli 299 katika mechi 287 alizocheza akiwa amevaa uzi
wa Real Madrid.Rekodi safi kabisa hii. Yaani magoli mengi kuliko idadi ya mechi
alizocheza.
8] Ana
magoli 36 sasa katika mechi 26 alizocheza msimu huu kwenye Ligi Kuu ya
Hispania.
Sasa hapo Messi anadeni kubwa kufikia rekodi hii
ya Ronaldo.!!!!
No comments:
Post a Comment