Wakazi wa kijiji cha
Mtambwe Kitongoji cha Shauri Moyo Wilaya ya Muheza wamelalamikia Shirika la Ugavi
la Umeme nchini Tanesco Walayani humo kwa kuunganishia umeme wakazi kiolela na
kusababisha kifo.
Wakazi hao wamesema wamekuwa wakitoa taarifa kwa uongozi wa Tanesco
wilayani humo baada ya kushuhudia nguzo imefungwa na inapeleka umeme katika
makazi ya watu bila kukamilika kwa baadhi ya vifaa bila kushughulikiwa hadi jumamosi
ya April 4 shoti ya umeme imegharimu maisha ya mtoto Aisha Kombo mwenye umri wa
miaka saba.
![]() |
Nguzo iliyogharimu maisha ya mtoto Aisha |
Mtoto huyo ambae ni mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mdote
alipoteza maisha wakati akicheza maeneo ya jirani na nguzo hiyo.
Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa mtoto Aisha, Kombo Ramadhani
Kombo amesema amesikitishwa sana na uongozi wa Tanesco kutokuwa makini katika
uwekaji nguzo za umeme ambazo ni hatari kwa watu walika zote.
Kombo amesema mtoto Aisha alikuwa akicheza katika eneo hilo wakati
kulikuwa na manyunyu ya mvua na kugusa waya uliotoka katika nguzo na kujikuta
akipoteza maisha ghafla.
Hata hivyo mwandishi wetu alifika katika eneo la tukio na kuona jinsi
nguzo hiyo ilivyokosa vifaa muhimu vya kuzuia umeme usishuke ardhini kutoka juu
ya nguzo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha shauri moyo Seffu Twenye amesema mara mbili
walitoa taarifa katika ofisi ya tanesco lakini hakuna utekelezaji wowote
uliofanyika hadi mtoto huyo alipokufa
Vilevile amesema sio nguzo hiyo peke yake ila anashangazwa sana jinsi
ya uunganunishaji wa umeme bila kuweka vikombe na kuomba uongozi wa shilika la
umeme Tanesco liwaeleze kama ni mbinu mpya ya uunganishaji wa umeme huo
unaoitwa umeme wa Obama.

No comments:
Post a Comment