Watu 10 wamefariki dunia kwa
ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni
wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.
Akizungumza na Mwandishi wetu Kamanda wa kikosi cha
usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili
ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.
Kwa mujibu wa Kamanda, gari dogo ilikuwa likitaka
kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la
Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.
Baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.
Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10
waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi
la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.

Taarifa toka eneo la
tukio zinaarifu kuwa Maiti pamoja na
majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya
Magunga iliyoko Wilayani Korogwe.

No comments:
Post a Comment