Bondia Alen Kamote wa Tanga atapanda
ulingoni mei 2 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga kukabiliana na Emilio Norfat
katika mpambano wa raundi 12 mbali na mpambano siku hiyo pia kutakuwa na
mapambano mengine makali moja ya mpambano wenye mvuto zaidi ni kati ya bondia
mwenye makazi yake mkoa wa Morogoro Cosmas Cheka atakaekabiliana na Said Mundi
kutoka mkoa wa Tanga.
Promota wa
mpambano uho Ally Mwazoa aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa
na mapambano mengine yatakayowakutanisha Jacob Maganga na Fadhili Kea
wakati Juma Mustafa akipamana na Ally Magoma, Saimon Zabroni akioneshana
umwamba na Hamisi Mwakinyo na Jumanne Mohamed na Bakari Shendekwa na
Zuber Kitandura na Rajabu Mahoja.
Mpambano huo
unafanyika jijini Tanga baada ya kutopata burudani ya mchezo wa masumbwi
kwa muda mrefu kidogo hivyo mpambano uho utafuraiwa na wakati wa Tanga na
vitongoji vyake
No comments:
Post a Comment