
Na Masanja
Mabula.PEMBA
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mkipi miliki Bw Mohammed Abdalla
Foum amesema elimu ya ujasiriamali inahitaji kutolewa ili
kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia dhana ya kujitegemea .
Amesema kuwa serikali imeweka fursa nyingi ambazo zinaweza
kusaidia vijana kuondokana na umaskini pamoja na matendo maovu ikiwemo ya
utumiaji wa madawa ya kulevya .
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na mwandishi wa habari
hizi ambapo pia amesisitiza haja kwa vijana kubuni miradi ambayo
itakuwa ni mkombozi kwao na familia zao .
Naye msaidizi afisa uendeshaji wa kampuni hiyo Mwalimu
Omar Khamis ali amezishauri taasisi zinazotoa mikopo , kutoa kipaombele
kwa vijana ambao wamejikusanya pamoja kwa lengo la kupambana na umaskini
wa kipato .
Hivyo amewataka vijana kuondoa dhana ya kutegemea ajira
kutoka serikalini , bali wajikusanye pamoja na kuanzisha mikundi vya
uzalishaji mali .
No comments:
Post a Comment