![]() |
|
Kiungo hatari
Simon Happygod Msuva(kulia)
|
Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara
imeendelea jana kwa mchezo mmoja wa kiporo kati ya Yanga na JTK Ruvu katika
Dimba la Taifa jijini DSM, mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 3-1 na
kupaa point 4 mbele ya timu ya pili kwenye msimamo wa ligi timu ya Azam Fc.
Katika mchezo huo mabao ya yanga
yamefungwa na Simon Msuva baada ya shuti kali alilopiga kushikwa na Amosi
Makwaya na refarii kutoa adhabu ya
Penalt iliyofungwa na Msuva mwenyewe dakika ya 35. Bao la pili limefungwa
kufuatia krosi ya winga hatari simon Msuva kumkuta Danny Mrwanda anayefunga na
kuiandikia Yanga goli la pili dakika ya 42.
Bao la tatu limepatikana kipindi
cha pili likiwekwa kimiani na Simon Msuva tena dakika ya 57.
Bao la kufutia machozi kwa upande wa JKT Ruvu lilifungwa na Samuel
kamuntu mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Kiungo Simon Happygod Msuva amefikisha mabao 11 na
kumpita aliyekuwa kinara wa ufungaji mshambuliaji wa Azam Didier Kavumbagu
mwenye magoli 10.
Kavumbagu raia wa Burundi
amekuwa akiongoza kwa ufungaji tokea kuanza kwa ligi hiyo.
MSIMAMO WA LIGI KUU
Rn
|
Timu
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
Gd
|
Pts
|
1
|
YANGA
|
19
|
12
|
4
|
3
|
28
|
11
|
17
|
40
|
2
|
Azam FC
|
18
|
10
|
6
|
2
|
25
|
12
|
13
|
36
|
3
|
SIMBA SC
|
20
|
8
|
8
|
4
|
25
|
14
|
11
|
32
|
4
|
KAGERA
SUGAR
|
19
|
6
|
7
|
6
|
16
|
17
|
-1
|
25
|
5
|
Coastal
Union
|
20
|
5
|
9
|
6
|
14
|
14
|
0
|
24
|
6
|
JKT
RUVU
|
20
|
6
|
6
|
8
|
16
|
19
|
-3
|
24
|
7
|
MGAMBO
|
19
|
7
|
3
|
9
|
13
|
19
|
-6
|
24
|
8
|
MTIBWA
SUGAR
|
18
|
5
|
8
|
5
|
18
|
18
|
0
|
23
|
9
|
MBEYA
CITY
|
19
|
5
|
8
|
6
|
14
|
16
|
-2
|
23
|
10
|
RUVU
SHOOTING
|
20
|
5
|
8
|
7
|
13
|
18
|
-5
|
23
|
11
|
NDANDA
FC
|
20
|
6
|
5
|
9
|
17
|
23
|
-6
|
23
|
12
|
POLISI MORO
|
20
|
4
|
9
|
7
|
13
|
17
|
-4
|
21
|
13
|
STAND UNITED
|
19
|
5
|
6
|
8
|
16
|
23
|
-7
|
21
|
14
|
T. PRISONS
|
19
|
2
|
11
|
6
|
13
|
20
|
-7
|
17
|
LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Aprili 4
Mtibwa Sugar v Stand United
Coastal Union v Tanzania
Prisons
Ruvu Shooting v Ruvu JKT
Ndanda FC v Mbeya City
Kagera Sugar v Simba (Mechi kuchezwa Kambarage, Shinyanga)

No comments:
Post a Comment