MKUU wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula, amevitaka vituo vya afya mkoani
hapa kutumia fursa ya mikopo itolewayo na Mfuko wa Bima ya Afya
(NHIF) ikiwemo vifaa tiba na madawa na kuweza kuwa msaada kwa wananchi
katika kupata huduma zilizo bora.
Akizungumza katika kikao cha
uhamasishaji mpango wa mikopo ya vifaa tiba kilichofanyika hospitali ya
Mkoa ya Bombo, Magalula amewaagiza waganga wakuu wa hospitali Mkoani na
Wilayani kuitumia nafasi hiyo itolewayo na Bima ya Afya.
Amesema kelele za wananchi
kulalamikia huduma mbovu zitolewazo katika vituo imezidi wakati ziko
fursa za kupunguza kero hizo kwa kukopa vifaa pamoja na ukarabati wa majengo
jambo ambalo ni nadra kuipata nafasi hii tuitumie vizuri.
Magalula amesema ni muhimu kuzichangamkia fursa hizi ili kupunguza kelele za wananchi
kulalamikia huduma mbovu zikiwemo uhaba wa madawa na vifaa katika hospitali
zetu
Mkuu wa mkoa ametoa agizo kwa
waganga wakuu wa hospitali zote za mjini na Wilayani kuhakikisha wanaitumia
ipasavyo fursa hii na kumaliza manung’uniko kutoka kwa wananchi juu ya
hospitali na vituo vyetu vya afya.
Pia amesema baadhi ya vituo vya
afya majengo yake yako katika mazingira hatarishi na mengine kufikia hatua ya
kutaka kuanguka na hivyo kuwaagiza kuchangamkia nafasi inayotolewa na
mfuko wa bima ya afya ili kuyanusuru majengo
mengi yako katika hali mbaya ikiwemo miundombinu ya kupitishia maji ni uchakavu
wa majengo jambo ambalo linaondoa taswira ya mazingira ya afya kwa wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa Taifa
Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa hapa , Ali Mwakababu, amesema mbali ya elimu na
matangazo mengi lakini hadi sasa ni vituo vichache ambavyo vimejitokeza kutaka
mikopo.
Mwakababu amesema elimu bado
inahitajika na hivyo kuitaka Wizara ya Afya Mkoa kutoa elimu kwa Waganga wakuu
wa Wilaya kuomba mikopo ambayo inaweza kusaidia kuimarisha huduma zao zikiwemo
matibabu na ukarabati wa majengo.
Meneja amesema mwaka 2007 Bima
ya Afya ilianzisha huduma ya kutoa mikopo ni vituo vichache ambavyo vimeomba
mikopo ya kukarabati majengo kwani majengo mengi ni chakavu na hayana vifaa
tiba mfano madawa ,na Ex ray amesema pia wanatoa.
Hata hivyo Meneja amewataka
waganga wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanamaliza changamoto wanazokabiliana nazo
katika vituo vyao lengo likiwa ni kuboresha huduma kwa wananchi.

No comments:
Post a Comment