Na Masanja Mabula aliyeko Mkoa
wa kaskazini -pemba.
Sheha wa shehia ya
majenzi wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba Bw Omar Pandu Kai amesimamishwa
kazi na mwajiri wake kutokana na tuhuma za kumbaka mwanawe wa kumzaa wa
kike anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 14.
Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa mkoa
wa kaskazini pemba mhe omar khamis othman ni kuwa uwamuzi wa kumusimamisha kazi
sheha hiyo zimekuja baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyombo vya usalama vya
mkoa huo .
Amesema kuwa sheha huyo amekiuka
maadili ya uongozi na kwamba amesimamishwa ili kupisha vyombo vya ulinzi viweze
kufanya kazi yake na kuvitaka kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria .
Mkuu huyo wa mkoa amesema hatakuwa
tayari kuona kuwa kiongozi wa serikali ambaye ataonekana kwenda akinyume na
taratibu za uongozi na kwamba atamwajibisha kwa mujibu wa sheria za utumishi wa
umma .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
sheha wa shehia mtemani wete juma mrisho magogo amesema kuwa kitendo
kilichofanywa na sheha huyo kimeshusha hadhi ya kazi yao .
Sheha magogo amesema kuwa ni vyema
vyombo vya sheria kufanya uchunguzi wake na kisha vichukuwe hatua kwa mujibu wa
sheria za nchi ili kudhibiti matendo ya udhalilishaji .
No comments:
Post a Comment