HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 23 March 2015

WATU 10 WAPANDISHWA KIZIMBANI TANGA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA POLISI KWENYE TUKIO LA AMBONI.



Silaha iliokamatwa kwenye tukio la Amboni.

Watu 10 wakazi wa jiji la Tanga wamefikishwa tena kwa mara ya pili mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga wakikabiliwa na kesi ya kuhusishwa na makosa matano tofauti kuhusiana na tukio la kuwanyang’anya Polisi SMG mbili zenye risasi 60 pamoja na kuua Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajenti Mohamed Kajembe.

Wahusika ni Mbega Seif (25) maarufu ‘Abuu Rajab, ambaye ni Mfanyabiashara mkazi wa Kiomoni, Rajabu Bakari (19) mwanafunzi mkazi wa Makorora, Ayubu Ramadhani (27) maarufu ‘Chiti’ ambaye ni Fundi umeme na mkazi wa Kona Z Kiomoni, Hassani Mbogo (20) maarufu Mpalestina ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa  Makorora, Mohamed Ramadhani (19)Mfanyabiashara na mkazi wa Makorora, Sadiki Mdoe (25)almaarufu kama kizota mkazi wa  Magaoni.

Wengine ni Saidi Omari (26)mfanyabiashara na mkazi wa  Magaoni tairi tatu, Nurdin Mbogo (27) Makorora, Ramadhan Mohamed (18)mfanyabiashara na mkazi wa  Donge pamoja na Omari Abdala (55) maarufu  ‘Ami’ mkazi wa Makorora Dunia Hoteli.
Walifikishwa mahakamani majira ya saa tatu za asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo ulinzi uliendelea kuimarishwa ndani na nje ya mahakama hiyo wakati shauri hilo likiendelea mahakamani.

Akizungumza mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Aziza Rutala Wakili wa serikali MariaClara Mtengule,alimwomba Hakimu kusogeza mbele kesi hiyo kutokana na upelelezi wa baadhi ya makosa yanayowakabili watuhumiwa hao kutokamilika.

Hata hivyo Rutala alikubaliana na ombi hilo na kusema kuwa kesi hiyo itatajwa tena Aprili 8, mwaka huu na kwamba washtakiwa wote wanatakiwa kwenda rumande kutokana na makosa yanayowakabili kutokuwa na dhamana.

Katika kesi la awali inayowakabili wakazi hao wa Jiji la Tanga, kosa la kwanza hadi la tatu linawahusisha washatakiwa namba moja mpaka nane kwa kuhusika kula njama ya kutenda kosa kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 384 sura ya 16 ya mwaka 2002.

Katika kosa la pili linadaiwa kutendeka mnamo Januari 26 mwaka huu katika mgahawa wa Jamali ulipo kati ya barabara ya nne naya tano jijini Tanga washitakiwa wote nane waliiba silaha moja aina ya SMG  namba za usajili 14303545 mali ya Jeshi la Polisi Tanzania na muda mfupi kabla ya kutenda kosa hilo walitumia visu kumchoma askari H 501 Mwalimu ili kupata silaha hiyo.

Ilielezwa kuwa kosa la tatu  la unyang’anyi wa kutumia silaha washtakiwa wote nane katika mgahawa wa Jamali uliopo kati ya barabara ya nne naya tano waliiba silaha nyingine yenye namba za usajili 14301230 SMG mali ya Jeshi la polisi Tanzania na kwamba muda mfupi kabla ya kutenda kosa hilo walimtishia kwa kutumia nguvu kumnyang’anya silaha askari polisi H Mansoor kinyume na sheria namba 287(a) ya kanuni ya adhabu kifungu 16 ya mwaka  2002.

Katika kosa la nne ambalo limemuhusisha mshatakiwa namba tisa Nurdin Mbogo wakili wa serikali Barasa alisema mnamo Februari 6 mwaka huu katika sehemu isyofahamika jijini Tanga mshtakiwa huyo akijua kuwa Hassan Mboko (Mshatakiwa Na. 4) alitenda kosa Septemba mosi 2014 na Januari 26 mwaka huu alimsaidia kumwezesha kukwepa kushtakiwa na kuadhibiwa kinyume na sheria namba 387 (I) na sheria namba 384 ya 2002.

Shtaka la tano liliwahusisha washtakiwa namba moja,mbili na namba 10 kwa kuhusika  kumuua Askari wa JWTZ Sajenti Mohamed Rashid Kajembe mnamo Februari 13 mwaka huu  katika Mapango ya Amboni Jijini Tanga kinyume cha sheria namba 196 na 197 ya makosa ya adhabu ya mwaka 2002 .

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.
Hii ni mara ya pili kw watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani hapo ambapo kwa mara ya kwanza walisomewa mashitaka yao Machi 9 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment