![]() |
| Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani R.T.O Abdi Isango akizungumza na baadhi ya madereva wa bodaboda jijini Tanga. |
WATU watatu wamepoteza maisha katika matukio matatu tofauti yaliyohusisha
ajali za barabarani mkoani Tanga.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Juma Ndaki amesema mnamo
tarehe 20/03/2015 mtembea kwa miguu asiyefahamika jina amegongwa na gari ambalo halikutambulika na
kufariki papo hapo katika kijiji cha kitumbi
kata ya Kwamkonga wilayani Handeni.
Tukio lingline ni la kijiji cha Mabalaga kata ya Mabalaga barabara ya
kuelekea Kwadiboma Wilayani Handeni, gari aina ya fuso lori lenye na T403 AHR lililokuwa
linaendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Abdalah, limepinduka na
kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Kamanda Ndaki amemtaja marehemu kuwa ni Selemani Rajabu mwenye umri wa
miaka 48 mkazi wa Gitu ambae kifo chake
kimetokana na kubanwa na mikungu ya
Ndizi ambapo watu wanne wamejeruhiwa, chanzo cha ajali hiyo ikiwa ni utelezi
barabarani uliotokana na mvua zinazo endelea.
Katika barabara ya Tanga–Muheza gari aina ya Toyota Pasho no T.885 CUD
likiwa na dereva Salehe Mayanjo alimgonga mwendesha baiskeli Twaha Omary mwenye
miaka 75 aliye fariki papo hapo.
Kaimu kamanda Ndaki amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza chanzo
cha ajari hiyo ambayo hakijafahamika na dereva anashikiriwa kwa hatua za
kisheria.

No comments:
Post a Comment