
Mshambuliaji wa
Emmanuel Emenike wa Fenerbahce amekuta akishindwa kujizuia na kulazimisha
afanyiwe mabadiliko na kutolewa nje hata kabla ya kipindi cha pili.
Katika
mechi hiyo ya Ligi kuu ya Uturuki dhidi ya wapinzani wao Besiktas, Emenike raia
wa Nigeria alilazimisha kutoka na kuvua jezi wakati mashabiki walipoanza
kumshambulia kwa maneno makali yakiwemo ya kibaguzi.
Mashabiki
hao walikuwa wakimzoea baada ya kushindwa kutuliza mpira mrefu aliopigiwa.

Hali
hiyo ilionyesha kumuudhi ingawa mashabiki hao pia walilalama kwamba msimu huu
amekuwa hana msaada kwa timu yao.
Pamoja
na kufanikiwa kutoka, Emenike alirudishwa na benchi la ufundi akiwemo kocha wa
timu hiyo ambaye hata hivyo baadaye alilazimika kumtoa baada ya kipindi cha
kwanza kwisha.
Ubaguzi
wa rangi umekuwa ukiendelea katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki ambayo ndiyo
nchini pekee duniani iliyo katika mabara mawili ya Asia na Ulaya.
Asilimia
kubwa ya Waturuki ni wale wenye asili ya Waarabu, lakini ajabu nao wamekuwa na
tabia hizo mbovu za hovyo za ubaguzi wa rangi.

No comments:
Post a Comment