Viongozi wa Ethiopia,
Misri na Sudan wamesaini makubaliano ya awali ya kusitisha mgogoro wa muda
mrefu unaohusu kugawana maji ya mto Nile na ujenzi wa bwawa kubwa zaidi barani
Afrika la kuzalisha umeme.
![]() |
| Viongozi wa Ethiopia, Misri na Sudan |
Viongozi hao walisaini
makubaliano hayo jana mjini Khartoum, Sudan.Kwa muda mrefu Misri imekuwa
ikipinga ujenzi wa bwawa kuu la Ethiopia la kuzalisha umeme, ikisema bwawa hilo
litaleta matatizo ya ukosefu wa maji kwa Misri.
Mwaka 2013, bunge la
Ethiopia liliridhia makubaliano mapya yenye utata ili kuchukua nafasi ya
mikataba ya kikoloni ambayo iliipatia Misri na Sudan viwango vikubwa vya maji
ya mto Nile. Aliyekuwa rais wa Misri wakati huo Bw Mohammed Morsi alisema
hataki vita, lakini hataruhusu upungufu wa maji nchini Misri kuathirika
kutokana na bwawa hilo.
Mrithi wa Bw Morsi, Rais
Abdul Fattah al-Sisi jana alisaini makubaliano na Waziri Mkuu wa Ethiopia
Halemariam Delasegn na Rais wa Sudan Omar al-Bashir kuhusu kugawana maji ya mto
Nile. Viongozi hao watatu wamekaribisha kusainiwa kwa makubaliano hayo katika
hotuba walizotoa mjini Khartoum baada ya kusaini.

No comments:
Post a Comment