Mazungumzo ya wakurugenzi nchini
Tanzania, ambayo ni jukwaa la sera linalokutanisha maofisa wakuu watendaji wa
karibu kampuni 100 zinazofanya biashara nchini Tanzania, jana yalieleza
wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
mkutano huo, ufisadi unaendelea kurudisha nyuma juhudi za maendeleo ya uchumi
wa Tanzania, na kwamba utendaji mbaya wa viongozi unaozidi kuongezeka unatoa
tahadhari pia vitendo vya wizi wa rasilimali za umma na kuhamisha fedha za umma
vinavyofanywa na maofisa kwa manufaa yao binafsi vimepunguza imani ya watu
katika uongozi, na kuendeleza kuibuka kwa utamaduni wa kutoadhibu wahalifu,
kupuuza sheria na kutukuza kukiuka maadili.
"Kwa sasa Tanzania ni nchi ya 119
kati 175 katika viwango vya rushwa, na kushuka kwa nafasi mbili katika miaka
miwili iliyopita"

No comments:
Post a Comment