Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA)
Kisiwani Pemba imetakiwa kuyatambua maeneo yote yenye vyanzo
vya maji ili iyawekea ulinzi dhidi ya uvamizi unaofanywa na baadhi
ya wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman wakati
akizindua wa Mradi wa maji katika Kijiji cha Chekea Shehia ya
Mtambwe Kaskazini Wilaya ya Wete ikiwa ni sherehe za maadhimisho ya
Wiki ya Maji Duniani .
Amesema
kuwa Mamlaka inapaswa kuyawekea ulinzi maeneo yote vya vyanzo vya Maji kwa
kuhakikisha kwamba inayawekea uzio ili kuziba mianya ya wananchi wanavamia
maeneo kuweza kuyafikia .
Katika
Hatuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Wete Bw Hassan Khatib
Hassan , amewataka wananchi wa Kijiji cha Chekea Mtambwe Kaskazini kuutumia mradi
huo wa maji kwa ajili kukuza uchumi na maendeleo yao na Taifa kwa Ujumla.
Mapema
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji (ZAWA) Pemba Juma Ali Othman amesema
kuwa mradi huo utaondoa changamoto ya uhaba wa maji iliyokuwa inawakabili
wananchi wa Kijiji hicho .
Ameeleza
kwamba Mamlaka imechimba Kisiwa katika Kijiji hicho chenye urefu wa mita 105 na
kinauwezo wa kutoa lita 960 kwa siku ambapo mahitaji ya wananchi wa Kijiji
hicho ni 450 kwa siku .

No comments:
Post a Comment