HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 4 March 2015

"YA MUNGU MENGI" MAPACHA WALIOUNGANA WAPATA NAFASI YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO.



PACHA walioungana kiwiliwili, Consolata na Maria Mwakikuti (18) wa Kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe wamefaulu mtihani wao wa kuhitimu kidato cha nne kwa alama sawa isipokuwa masomo mawili.

Ufaulu wao wa alama ya credit 2.0, huku wakiwa wamefanya vizuri katika Kiingereza na Baiolojia, umekuja wakati wanafunzi wengi wa shule ya Sekondari Maria Consolata iliyoko mkoani Njombe, wakiwa wamefanya vibaya katika matokeo ya mwaka jana.
Kutokana na alama walizopata, zinawawezesha Maria na Consolata kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano, Julai mwaka huu.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wasichana hao walioko kijijini kwao Ikonda , walisema masomo waliyotofautiana katika ufaulu ni Kemia ambalo Maria amepata C na Consolata D na Kiingereza ambalo Maria amepata B na Consolata B+.
Katika matokeo hayo ambayo kila mmoja alikuwa na namba yake ya mtihani (Maria-S. 283/0004 na Consotala S 283/0009), masomo ambayo wamelingana ni Uraia wakiwa na E, Historia C, Jiografia E, Kiswahili C, Baolojia B na Hesabu C.

“Tumefurahia sana kufaulu, tutaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita shule hapo Julai,tutasoma mchepuo wa CBG (Kemia,Biolojia na Jiografia) au HGL, (Historia,Jiografia na Kiingereza),” alisema Consolata.
Aliendelea kusema, “tunategemea kwenda Shule ya Sekondari ya Udzungwa iko karibu na shule tuliyosoma kidato cha kwanza hadi cha nne ya Maria Consolata kule Kidabaga, Kilolo.”
Kwa upande wake Maria, alisema amefurahi na matumaini yao ni kujitahidi kusoma kwa bidii zaidi wafaulu na kujiunga na elimu ya juu.
“Nimefurahi mimi na Consolata, tulipigiwa simu na walimu wakatuambia matokeo yetu, mama yetu mlezi amefurahi na Mungu akipenda tutaanza masomo mwezi Julai; Ya kidato cha tano”,alisema Maria ambaye kwa mujibu wake, wana ndoto za kuwa wahasibu.
Alisema kwa sasa wako likizo wamepumzika nyumbani kwao Ikonda chini ya uangalizi wa mama yao mlezi na dada yao msaidizi, Magdalena Mbilinyi .Wanatarajia kurudi Kilolo, kwenye Kituo cha Nyota ya Asubuhi kati ya Machi 7 na 14, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment