WATU wanne akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee wawili wa kimila wa kijiji hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusu kuuawa kwa wazee wawili mtu na mkewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
David Misime
|
Alisema watu waliokamatwa wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mume na mke, Peter Kaluli (85) na Kaila Kaluli (80) wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao ya tembe.
Aidha alisema kwamba watu hao waliuawa kwa kuangushiwa ukuta wa nyumba yao kisha kuchomwa moto. Pia wanatuhumiwa kuhusika na kubomoa nyumba nyingine mbili za tembe za kaya hiyo.
Alisema tukio hilo lilitokea kwenye kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda, Kata na Tarafa ya Mlali wilayani Kongwa. Kwenye tukio hilo watu hao walifanya uharibifu mwingine kwa kuwaua nguruwe mmoja na kumkata miguu ng’ombe.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji na uharibifu huo ni imani za kishirikina wakiwatuhumu vikongwe hao kuwa wanazuia mvua kunyesha.
No comments:
Post a Comment