POLISI mkoani Katavi imewakamata wakazi
wawili wa mkoa wa Mwanza wanaotuhumiwa kukodiwa kumuua mkazi
wa mjini Mpanda wakiwa na risasi za sialaha nzito za
SMG na SAR na bunduki aina ya shotgun na risasi zake
tano kinyume cha sheria .
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa
hao kuwa ni pamoja na Vicenti Yusuph (31) na Mkuki Juma miaka
(25)ambao pia walikutqa na sare za jeshi .
Kamanda
Kidavashari hata hivyo hakuwa tayari kumtaja mkazi huyo
wa mjini Mpanda. Alifafanua kuwa tukio hilo lilitokea jana saa tisa
na nusu jioni katika eneo la Mjimwema mjini Mpanda.
“Kukamatwa
kwa watuhumiwa hawa kumewezekana baada ya kupata
taarifa za siri kutoka kwa raia wema……. Hivyo tulitega
mtega na tukafanikiwa kuwanasa a walipohojiwa walikiri kuwa
walikodiwa kumuua mkaziwa mjini Mpanda (jina limehifadhiwa)
Kadhalika
walikiri kuwa walikuja mkoani hapa ili kufanya
uhalifu kwa kuvamia maeneo ya minada na kupora fedha “
alibainisha.
Kwa mujibu
wa Kidavashari watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awali wa shauri lao
kukamilika.
Katika mkasa
mwingine , kwa mujibu wa kamanda Kidavashari Polisi mkoani humo
inamshikilia mkazi wa kijiji cha Katumba wilayani Mlele ,Hamadi Said
miaka (29) akiwa na ngozi ya chui yenye thamani ya
zaidi ya Sh milioni 5.7 ya chui aliyeuawa.
Kidavashari
alidai kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana mchana katika Mtaa wa
Kawajense alitafuta mnunuzi wa nyara hiyo ya Serikali ambapo atafikishwa
mahakamani mara tu upelelezi wa awali wa shauri lake
utakapokamilika .
No comments:
Post a Comment