Na Masanja Babula
.PEMBA.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar inaunga mkono juhudi
zinazochukuliwa na taasisi ya Kimataifa ya Global Peace Foundation katika
kuhimiza amani na utulivu Duniani.
![]() |
| Maalim Seif |
Maalim Seif amesema hayo jana wakati alipokuwa na mazungumzo na ujumbe
kutoka jumuiya hiyo, ulioongozwa na Rais wake, James Flynn huko ofisini kwake
Migomnani mjini Zanzibar.
Amesema Dunia inakabiliwa na matukio
mengi yanayo hatarisha amani na utulivu, hivyo mchango wa jumuiya hiyo ni
muhimu katika kupatikana ufumbuzi wa migogoro hiyo na kuwezesha watu kuishi
katika hali ya utulivu na kuvumiliana.
Maalim Seif amesema kwa upande wa
Zanzibar kuna kila sababu ya kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa
watu wake kuishi kwa kuvumiliana, licha ya kuwepo watu wenye imani tafauti za
kidini, na itikadi za kisiasa.
Amesema hatua hizo zitawaepushia
kuchukua maamuzi yasiyokuwa ya busara yanayosababishwa na vijana kupoteza
mweleko wa kimaisha ambapo matokeo yake ni amani na utulivu wa nchi kuvurugika.
Naye Rais wa Jumuiya hiyo, James Flynn
amesema nguvu kubwa wanazielekeza kusaidia ujenzi wa familia zinazozingatia
maadili mema, pamoja na kushirikiana na Serikali za nchi tafauti kusimamia
utawala bora ambao una umuhimu wa kipekee katika kudumishwa amani na utulivu.

No comments:
Post a Comment