Zaidi ya Wanakijiji 500 wa Kijiji
cha Kigombe kilichopo kata ya Kigombe Wilayani Muheza mkoani Tanga wakiongozwa
na viongozi wao wameshiriki kwenye zoezi la msaragambo wa kusafisha maeneo
mabilimbali ya kijiji hicho hasa kwenye fukwe za bahari ya hindi ambapo
takataka hutupwa kwa wingi na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho.
![]() |
|
Mdau wa Usafi kijijini
hapo Bw Athumani Mtoro
(watatu kutoka kushoto)
akiwa na wadau wengine
wa usafi namaendeleo
kijijini hapo.
|
Zoezi hili limefanikisha
kukusanywa kwa zaidi ya tani moja ya taka huku zaidi ya kg 900 zikikusanywa
upande wa fukwe za habari pekee.
|
Fukwe za Kigombe
|
Akizungumza na waandishi
wa habari mdau wa Usafi kijijini hapo Bw Athumani Mtoro amesema wanawashukuru
wawekezaji wa Hoteli ya Peponi Beach Resort ambao ndio walio andaa na kuratibu
zoezi hilo kwani limeamsha ari ya wananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao na
kuacha tabia ya kutupa taka hovyo.

No comments:
Post a Comment