Zaidi ya Wanafunzi 200 kutoka shule 10
za Sekondari jijini Tanga watashiriki kwenye michuano maalum ya Riadha kwa
ajili kuchangisha fedha za kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima na Wajane
vya Chumbageni, Makorora na Mwakizaro jijini hapa.
Mbio hizo zitakuwa za umbali wa km 8
kituo cha kwanza kikiwa ni Shule ya Sekondari Popatlal kupitia barabara ya
Raskazoni kwenda barabara ya Tanga Beach kurudi mpaka Shule ya Old Tanga ambapo
kutakuwa na kituo cha ukaguzi na kurejea tena Shule ya Sekondari Popatlal kwa
barabara ya Bombo kilipo kituo cha mwisho.
Akizungumza na mtandao huu Mratibu wa Mbio hizo Mr Ropert kutoka shule ya Sekondari Popatlal amesema shule
kumi zimethibitisha kushiriki huku mashirika binafsi na yauma yakiunga mkono na
yakiruhusiwa kushiriki mbio hizo ili kuongeza chachu ya mashindano.
Shule
shiriki ni Usagara Sec, Eckenforde Cambridge Sec,Chumbageni Sec, Toledo Sec,
Nguvumali Sec, Mnyanjani Sec, Mikanjuni Sec, Old Tanga Sec,Mkwakwani Sec na Wenyeji
Popatlal ambao ndio wameandaa mashindano hayo.
Mshindi wa kwanza atazawadiwa Baiskeli
wa pili atapata Redio na watatu atajinyakulia Pea moja ya Viatu vya michezo.
No comments:
Post a Comment