HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 27 March 2015

“Click hapa kwa story za Bungeni” KWA HILI WAANDISHI WATAENDELEA KUWA MAADUI WA SERIKALI.



Dodoma. Mvutano mkali uliibuka jana bungeni wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha Muswada wa Takwimu wa mwaka 2013, baada ya wabunge kuupinga. Muswada huo una kipengele kinachotoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini isiyopungua Sh10 milioni kwa mtu au chombo cha habari kitakachofanya makosa ya kutoa takwimu zisizokuwa sahihi.

Mbunge wa Ubungo (Chadema)
John Mnyika

Wabunge hao waliufananisha muswada huo na miswada miwili ya habari ya mwaka 2015 ambayo itawasilishwa bungeni Jumanne chini ya hati ya dharura kwa usiri uliopo na mpango wa kuiwasilisha bila wadau kushirikishwa.

Awali, muswada wa Takwimu uliwasilishwa kwenye mkutano wa 17 wa Bunge uliofanyika Novemba mwaka jana na wabunge wakapinga vifungu vinavyobana waandishi wa habari kuhusu eneo la takwimu, ndipo Serikali ilipoamua kuutoa kwa maelezo kuwa inakwenda kuurekebisha hadi ilipourejesha jana na ukapitishwa kwa mbinde.

Jana, Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha muswada huo, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alihoji juu ya kifungu hicho kinachotoa adhabu kali na Serikali kujibu kuwa imeshakifanyia marekebisho.

Hata hivyo, Mnyika hakukubaliana na maelezo hayo, bali alisema kifungu hicho hakijafanyiwa marekebisho yoyote na Serikali na adhabu bado inaendelea kuwa kali.
Mnyika aliungwa mkono na mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya aliyehoji, “Iweje Serikali iweke kinga kwa mtumishi wa Serikali anayetoa taarifa zisizo sahihi lakini ikaacha kuweka kwa mwandishi anayepewa taarifa hizo zisizo sahihi na ofisa huyo wa Serikali?”


Maelezo ya Bulaya yalimfanya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju kusimama na kusema kwa kifupi kuwa “mwandishi atakwenda kujieleza mahakamani au polisi.”
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI

No comments:

Post a Comment