Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anaweza kumchukua Straika wa
Tottenham Emmanuel Adebayor kwa Mkopo kwa ajili ya Msimu ujao.
![]() |
| Emmanuel Adebayor "mtata" |
Gazeti la Uingereza
Daily Mirror limeripoti kuwa Mourinho anamtaka Adebayor Stamford Bridge ili
kuchukua nafasi ya Didier Drogba ambae anatafakari kustaafu mwishoni mwa Msimu.Mourinho
anahitaji Straika wa 3 wa akiba ili kuchukua nafasi za Diego Costa na Loic Remy
endapo wataumia au kufungiwa.
Ikiwa Adebayor atatua
Chelsea hii itakuwa mara ya pili kwake na Mourinho kuungana kwani Miaka Minne
iliyopita Mourinho akiwa Real Madrid alimchukua Adebayor kwa Mkopo kuziba pengo
la Majeruhi Gonzalo Higuain na huko Straika huyo aling'ara na kufunga Bao 8
katika Mechi 22.Hivi sasa Adebayor, Straika kutoka Togo mwenye Miaka 31, hana
namba Spurs iliyo chini ya Meneja Mauricio Pochettino.
Mwezi Januari Adebayor
nusura ahamie kwa Mkopo West Ham lakini Mkuu wa Spurs, Daniel Levy, akaweka
ngumu kwa kuitaka West Ham ilipe Mshahara wote wa Mchezaji huyo wakati akiwa
huko kwa Mkopo kitu ambacho West Ham walikikataa.
![]() |
| Paul Pogba "fundi" |
Zipo ripoti kuwa Manchester United itatumia zaidi ya Pauni
Milioni 100 mwishoni mwa Msimu ili kuimarisha Kikosi chao.
Man United, ambao sasa
wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England nyuma ya Chelsea, Man City na Arsenal,
mwanzoni mwa Msimu walitumia zaidi ya Pauni Milioni 150 kununua Wachezaji wapya
wakiwemo Radamel Falcao, aliechukuliwa kwa Mkopo kutoka AS Monaco, na Angel Di
Maria, ambao hawajaonyesha cheche zozote huko Old Trafford.
Ripoti zimedai sasa Van
Gaal atalenga Wachezaji Vijana waliokomaa na mahiri kwenye Klabu na Timu zao za
Taifa.Miongoni mwa walengwa wake waliotajwa kwenye Ripoti hiyo ni Beki wa
Germany na Klabu ya Borussia Dortmund, Mats Hummels, mwenye Miaka 26, na
Chipukizi wa Kimataifa wa Holland, Memphis Depay.
Wengine ni Kiungo wa
France na Juventus, Paul Pogba ambae alitokea Timu ya Vijana ya Man United.Pia
watajwa wengine ni Fulbeki wa FC Porto, Danilo, na yule Mbrazil wa Barcelona
Dani Alves.Pia waliwahi kutajwa Garreth Bale anaesakamwa na Mashabiki wa Klabu
yake Real Madrid lakini mwenyewe amesisitiza kubakia Madrid.


No comments:
Post a Comment