![]() |
| Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij |
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo asubuhi imefanya mazoezi ya
mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya taifa ya Malawi (The Flames) mchezo
utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Tiketi za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika
vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa
mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu
maalum.
Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa
viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika
wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo.
Akiongea na waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La
Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum
Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na sasa kilichobakia ni
mchezo wenyewe wa kesho.
Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini
wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho
tu kushuka dimbani kusaka ushindi.
Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu
waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi
kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.
Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili
jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini
Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda),
mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba
Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka
Mwanza.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:
Post a Comment